Vijana Mnaotafuta Ajira jifunzeni kuwadanganya walinzi!!

Vijana Mnaotafuta Ajira jifunzeni kuwadanganya walinzi!!

Chinedu5

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2015
Posts
784
Reaction score
2,818
Habari za muda huu wana jamii?

Matumaini yangu wote mpo salama,wale msio salama basi Mwenyezi Mungu awape nguvu kwenye kipindi hichi kigumu mnachopitia.

Niingie kwenye mada moja kwa moja.Leo wakati nipo ofisini mida ya saa 8 hivi,nilitembelewa na mgeni hivyo nikashuka chini kuonana nae, sasa wakati natoka pale getini kwa mlinzi kuna dustbin,ndani kulikua na bahasha za kaki kama 2 hivi na makaratasi kibao yakiwa yamechanwa chanwa,zile karatasi zilikua cv za watu na copy ya vyeti..,aisee roho iliniuma sana😨😪😔

Niwasaidie tu ma graduates,na vijana wenzangu mnaopambana kutafuta ajira na sehemu za kujitoleo hakikisheni HAMUACHI CV ZENU KWA WALINZI.. nasema hivyo kwa sababu nmeona baadhi ya walinzi na ma secretary wengi wana roho mbaya huwa hawazifikishi sehemu husika.

Nini kifanyike?? kabla hujapeleka cv yako kwenye kampuni hakikisha unafanya tafiti ya kutosha kama ni mkurugenzi au Hr,jitaidi ujue jina lake lote na maeneo anayopenda kutembelea,yani uwe na details zake kidogo tu zitakusaidia.

Sasa fanya hivi,ukifika apo kwa mlinzi au secretary usiulize meneja,hr au mkurugenzi, wew taja jina lake mfano "namuulizia mh chinedu nmemkuta? " au "naweza kumuona mh chinedu? "apa lazima watakuuliza una appointment nae? Hapa wewe sema ndio(kwa kujiamini sana) na hapa uwe mjanja kidogo,unaweza ukaongeza na "nilikutana nae last week nikaongea nae akasema nije ofisini".

Lazima atapiga simu kuulizia kwa huyo Hr kama anakufahamu, atajib tu simfahamu lakini kwa sababu umesema wewe unamfahamu na ulikutana nae basi atakua curious na wewe lazima akuruhusu uingie ofisini kwake, ukishafika sasa ndo unaanza kujieleza shida zako!!

Nimalize kwa kusema atu siku zote Boss hana shida,mchawi chawa😂😂😂2013 niliwahi kujibiwa na mlinzi kwenye kampuni fulani "sasa hivi hatuajiri"😂😂😂😂
 
Shida waomba ajira, wanaenda kuomba ajira zenye vyeo vikubwa kuliko vya wanaowakuta getini au mapokezi. Waombaji hao hujiona "matawi" na kuleta zeleu. Shida ndio huanzia hapo.
 
Ulimuuliza kwanini labda CV za watu zipo kapuni na zimechanwa? Au alitamba mwenyewe kuwa nimewachania? Imenigusa mno hii habari
 
Unakuja na mtepesho..kiduku..kimini..na mchuchumio..ili uje uwe boss wangu nooo..naichana chana....hayo ni maneno ya walinzi na masekretari.

#MaendeleoHayanaChama
 
2017 nilifukuzwa getini mwa kampuni kubwa nchini la magazeti na walinzi kisa niliwaambia natafuta kazi...kesho yake nikamvizia mmoja wa maboss wakiwa wanaingia getini CV zangu zikafika...niliporudi tena wakaniambia Watanivunja mi nikawaonyesha electronic card ya kufungulia electronic doors za mule ndani walipigwa butwa ila baadaye walinzi walikuja kuwa jamaa zangu kishenzi kiasi cha kuwa ingawa kila mwajiriwa ilikuwa lazima akaguliwe before kuingia walikuwa hawanikagui tena huku baadhi ya maboss wangu wakikaguliwa.
 
Shida waomba ajira, wanaenda kuomba ajira zenye vyeo vikubwa kuliko vya wanaowakuta getini au mapokezi. Waombaji hao hujiona "matawi" na kuleta zeleu. Shida ndio huanzia hapo.
Hata hivyo, bado kuichana sio suluhu bora ukatae kumpokelea tu ajue
 
Ulimuuliza kwanini labda CV za watu zipo kapuni na zimechanwa? Au alitamba mwenyewe kuwa nimewachania? Imenigusa mno hii habari
Yaani nilichukua na kusoma vipande vipande hivyo,sasa hivi ofisini kwetu wametuletea hawa Suma jkt,ni vijana wa hovyo sana
 
Ni ngumu kumeza jamani, Mlinzi? Achane CV za watu? Mhhh
Mimi mwenyew nmeshangaa sana, najua hawa watu wengi wanaroho mbaya ila. sikuwaza ipo siku watafanya hili
 
Unakuja na mtepesho..kiduku..kimini..na mchuchumio..ili uje uwe boss wangu nooo..naichana chana....hayo ni maneno ya walinzi na masekretari.

#MaendeleoHayanaChama
Unamchania mtu cv zake leo kesho unaenda kuomba wewe kazi unamkute yeye ndo Hr apo
 
2017 nilifukuzwa getini mwa kampuni kubwa nchini la magazeti na walinzi kisa niliwaambia natafuta kazi...kesho yake nikamvizia mmoja wa maboss wakiwa wanaingia getini CV zangu zikafika...
Ulitumia mbinu nzuri sana,hawa watu sijui wanakuaga na roho gani😂😂😂
 
Back
Top Bottom