Vijana Mnaotafuta Ajira jifunzeni kuwadanganya walinzi!!

Vijana Mnaotafuta Ajira jifunzeni kuwadanganya walinzi!!

anahis akipelekea cv yako utatoka kimaisha umwsche yeye kolokoloni
 
Habari za muda huu wana jamii?

Matumaini yangu wote mpo salama,wale msio salama basi Mwenyezi Mungu awape nguvu kwenye kipindi hichi kigumu mnachopitia.

Niingie kwenye mada moja kwa moja.Leo wakati nipo ofisini mida ya saa 8 hivi,nilitembelewa na mgeni hivyo nikashuka chini kuonana nae, sasa wakati natoka pale getini kwa mlinzi kuna dustbin,ndani kulikua na bahasha za kaki kama 2 hivi na makaratasi kibao yakiwa yamechanwa chanwa,zile karatasi zilikua cv za watu na copy ya vyeti..,aisee roho iliniuma sana😨😪😔

Niwasaidie tu ma graduates,na vijana wenzangu mnaopambana kutafuta ajira na sehemu za kujitoleo hakikisheni HAMUACHI CV ZENU KWA WALINZI.. nasema hivyo kwa sababu nmeona baadhi ya walinzi na ma secretary wengi wana roho mbaya huwa hawazifikishi sehemu husika.

Nini kifanyike?? kabla hujapeleka cv yako kwenye kampuni hakikisha unafanya tafiti ya kutosha kama ni mkurugenzi au Hr,jitaidi ujue jina lake lote na maeneo anayopenda kutembelea,yani uwe na details zake kidogo tu zitakusaidia.

Sasa fanya hivi,ukifika apo kwa mlinzi au secretary usiulize meneja,hr au mkurugenzi, wew taja jina lake mfano "namuulizia mh chinedu nmemkuta? " au "naweza kumuona mh chinedu? "apa lazima watakuuliza una appointment nae? Hapa wewe sema ndio(kwa kujiamini sana) na hapa uwe mjanja kidogo,unaweza ukaongeza na "nilikutana nae last week nikaongea nae akasema nije ofisini".

Lazima atapiga simu kuulizia kwa huyo Hr kama anakufahamu, atajib tu simfahamu lakini kwa sababu umesema wewe unamfahamu na ulikutana nae basi atakua curious na wewe lazima akuruhusu uingie ofisini kwake, ukishafika sasa ndo unaanza kujieleza shida zako!!

Nimalize kwa kusema atu siku zote Boss hana shida,mchawi chawa😂😂😂2013 niliwahi kujibiwa na mlinzi kwenye kampuni fulani "sasa hivi hatuajiri"😂😂😂😂
hii nii kweli kabisa mkuu, nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nnilikuwa na shida na HR wa Twiga cement pale Wazo...nilivyofika pale kwanza nilimpiga mlinzi mkwara wa maana!! alini escort mwenyewe mpaka kwa hr, na tatizo langu likatatuliwa kabisa.
 
Sasa nani atakuruhusu umuone mkurugenzi.? mwisho wa siku kuacha cv kwa mlinzi ni kwamba huna jinsi inabidi iwe hvy hasa kama huna connection
ushaambiwa na mtoa mada hapo juu ni nini ufanye, tafuta jina au connection yoyote na muhusika.
kila kitu kinahitaji sana kujiamini.
Kuna mlinzi mmoja w kampuni ya Zara,nilienda pale kwa lengo la kuoanana naMkurugenzi, nilivyofika tu akafikiri natafuta kazi.
Cha kwanza nilimuuliza Mama yupo? wala sikusema bossi, jamaa akauliza mama yupi? nikatajia jina la huyo mkurugenzi, alihamaki sana na nilivyojiamini alijua kabisa nina uhusiano wa karibu na huyo bossi. Kiulaini nikaingia. kifupi huwa sizuiliwi na mlinzi au secretary nikitka kuoanana na mtu ofisini kwake, labda ukute hayupo wakati huo na si vinginevyo.
 
Sio tu walinzi na masecretary pia maana wana roho ngumu hao[emoji23]
 
Mbona walinzi tuko poa sana. Ukija job getini ukikutana na mimi lazima utatamani uje kila siku.
Nadhani njaa na elimu duni ndio hupelekea roho mbaya.
 
ushaambiwa na mtoa mada hapo juu ni nini ufanye, tafuta jina au connection yoyote na muhusika.
kila kitu kinahitaji sana kujiamini.
Kuna mlinzi mmoja w kampuni ya Zara,nilienda pale kwa lengo la kuoanana naMkurugenzi, nilivyofika tu akafikiri natafuta kazi.
Cha kwanza nilimuuliza Mama yupo? wala sikusema bossi, jamaa akauliza mama yupi? nikatajia jina la huyo mkurugenzi, alihamaki sana na nilivyojiamini alijua kabisa nina uhusiano wa karibu na huyo bossi. Kiulaini nikaingia. kifupi huwa sizuiliwi na mlinzi au secretary nikitka kuoanana na mtu ofisini kwake, labda ukute hayupo wakati huo na si vinginevyo.
swala la msingi ni kujiamini, na ukiwa na details za muhusika utajiamin zaidi
 
Mbona walinzi tuko poa sana. Ukija job getini ukikutana na mimi lazima utatamani uje kila siku.
Nadhani njaa na elimu duni ndio hupelekea roho mbaya.
Yah sio wote, kuna mama alikua mlinzi apa ofisini kwetu kabla kampun yao haijatolewa, yule mama alikua mwema sana, ali tu treat kama wanae na sisi kama mama etu, ila hivi vilivyokuja vya ismail ni shida
 
Hata hivyo, bado kuichana sio suluhu bora ukatae kumpokelea tu ajue
Kuna dada mmoja wa kampuni ya saruji alikataa kuipokea , na kuniongelea maneno ya kukatisha tamaa kwamba saizi hamna kazi, nikamwambia Basi naomba nionane na Hr, akakataa akasema hapa ndo imefika , mwisho wa siku tuliishia kupanikishana nusra tuxichape ngumi, ila niliishia kuondoka na CV zangu.
Mana akazipiga muli kuwa received hafu akaenda kuziweka kwenye dust bin.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma btn 2013 mshikaji wangu mmoja minimum wage Civil aliwahi kwenda kuomba Ajira tena internship pale DAWASA.. wakati ule hawakuwa wanarecruit via AjiraPortal.. Jamaa kapiga pamba fresh kufika getini walinzi wakamletea Nongwa.. akawaambia anatoka Ikulu anahitaji kuonana na Menejaa Mzungu mmoja hivi, wakaingia upepo wakamruhusu.

Jamaa kuingia kwanza ndani kuna geti mbili.. na ofisi ya meneja yenyewe haijui.. ikabidi ajieleze kwa mama mmoja mtu mzima ndo akaelekezwa.

Buum Jamaa alipata kazi siku hiyo hiyo.. Hapa tunavyoongea Mshikaji ni CEO wa DAWASA.
 
Miaka mitano iliyopita nilienda shule moja kuomba kazi, sasa nikakutana na secretary, nikamwambia namtafuta mkuu wa shule, kaniuliza shida gani, nikijua nia yake ni njema nikamjibu natafuta kazi ya kufundisha, akajibu kwa sasa hakuna kazi labda uache tu barua yako kazi ikipatikana tutakujulisha, nikakomaa nataka kuongea na mkuu wa shule, akalazimika kunionyesha ofisi yake, sasa bana ile kufika tu, wala mkuu wa shule hakutaka kupokea barua yangu, alichofanya ni kunipiga interview moja kwa moja, nami sikukopesha nilimwambia nimeambiwa kuwa hakuna nafasi ila nimekuja kuacha cv nafasi ikipatikana unifikirie, akanijibu aliyekwambia hakuna nafasi yeye kajuaje? Tunatafuta mwalimu wa Phy/math mwezi wa tatu sasa na tuna mpango wa kuanzisha A- level na walimu hakuna, nikajua baada ya mim kuondoka lazima iwe kesi maana jamaa alionyesha kukasirika. Kwa kumalizia tu, offer yao ilikuwa 700k na mimi nilikuwa nataka 900k so sikuchukua kazi yao[emoji23]
 
Lakini yote 9. 10 amini usiamini mlinzi mpaka kufikia kuchana CV za watu ujue ameshapewa hiyo older kutoka juu kwa mkurugenzi mwenyewe. Kwamba kwa sasa sihitaji mtu wa kumuajiri,kwa hiyo wakifika hapa pokea halafu zisambaratishe. Vinginevyo mlinzi hawezi kuwa jasiri bila kupewa ujasiri
 
Mwaka juzi Kuna kampuni wanakazi kwenye mafuta na gesi nilienda kuonana na boss nikafanikiwa ila alikuwa ndio yupo getini tukaongea machache na akaniambia kesho leta CV utampa mlinzi au secretary.

Kesho nikapeleka CV nikamkuta mlinzi Kisha nikampa secretary ni mwanaume ile kaipokea kaanza maneno ya kejeli "Jamaa pambana mtaani pagumu, kazi zimekuwa ngumu kupatikana, daah umesomea haya mambo na maneno kibao".

Nilivyoona kimya nikajua jamaa CV hakufikisha, sikupata muda Tena kurudi ofisi Ile.
 
Back
Top Bottom