Vijana Msijidanganye: Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa

Naona waajiriwa mnatiana moyo huku mkijua maisha yenu ni magumu na mshahara hautoshi, discipline ni kila mahali na siyo kwenye kujiajiri tu. Nyie endeleeni kutoa Muda wenu kwa boss na kumtajirisha huku yeye akiwapangia hela za kuwapa ili mkidhi mahitaji yenu ya kula na kuvaa. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Stress ziko kila kona na siyo kwenye biashara tu, hivyo iyo "displini" siyo kwenye kujiajiri tu. Biashara mjini ndo zina mapato, mishahara imejaa makato.

Hamjiulizi kwanini 75% ya waliojariwa wana maisha magumu zaidi kuliko waliojiariji?

Biashara yeyote mwanzo lazima iwe ngumu na nguvu nyingi huitajika ili kuipush..ila ikisimama utaona matunda yake, ila ajira kwanzia unaajiriwa hadi unakuja kuacha mwanzo mwisho ni mateso tu hasa ya kifikra na kiuchumi. Siku zote mshahara huwa hautoshi na huo ndo ukweli.

Ajira haitakupa utajiri wowote ule na ndio maana tunaona wazee wengi wakistaafu wanakufa na presha maana hakuna chochote wanachomiliki kwa kuwa waliuza Muda wao mwingi kwa boss huku wakilipwa percent ndogo ya Muda wanaotoa.
Hapa suala ni desiplini na ina apply kote kote kwenye ajira na kujiajiri. Lakini desiplini ya kuajiriwa haitokupa chochote zaidi ya sifa tu kama vile mfanyakazi bora, boss atakupamba na kamshahara kazuri ili aendelee kutumia Muda wako.
Kuna mbinu moja sisi maintaprinyua huwa tunatumia inaitwa "teka moyo wake mwachie akili yake" hahaha hapo mtajiongeza wenyewe, kujiajiri kuna ongeza akili zaidi kuliko izo ajira huwa zinadumaza akili kabisa.

Twende mbele turudi nyuma .."hakuna mtumwa m'baya kama kujiona uko huru"
 
Ukifika stage ya kuajiri watu unaweza relax kwanini mkuu? Huu ndio mwanzo wa kupigwa changa la macho alafu baadaye mtu anaanza kulalamika humu JF.
Mkuu inaonekana kabisa hujawahi kufanya biashara yeyote ile na tangu umemaliza chuo wewe ni mtu wa kuajiriwa tu. Kuna kitu kinaitwa system na ndio maana pesa inaweza kufanya kazi kwa ajili yako wewe ukiwa umerelax tu. Tatizo wafanyakazi wengi kama wewe mnafanya kazi kwa ajili ya pesa. Waliojiari kama sisi tunajenga 'mfumo' ambapo pesa inakufanyia kazi, unaweza wewe usiwepo na pesa inaingia kama kawaida.

Shtuka bro, 11 years umemaliza chuo na bado umeajiriwa. Bado una nafasi ya kufikiri upya
 
Dogo comments zako kadhaa hapo juu nimezikubali. Uko vizuri tatizo lako ni kushabikia lile timu bovu tu!
 
Magufuli hawezi kuuza Nchi ni Mzalendo haswa Usimfananishe na wale waliotumwa na Wazungu.
 
Dogo comments zako kadhaa hapo juu nimezikubali. Uko vizuri tatizo lako ni kushabikia lile timu bovu tu!
Hahaha hapo kwenye timu tutatofautiana sana. Kumbuka Chelsea ni timu ya baba, timu ya mama, timu ya babu na bibi pia ..kwanini mimi niwe tofauti nao? Hahaha unataka nipate laana mkuu..

Anyway shukrani mkuu.
 
Dogo comments zako kadhaa hapo juu nimezikubali. Uko vizuri tatizo lako ni kushabikia lile timu bovu tu!
Hahaha hapo kwenye timu tutatofautiana sana. Kumbuka Chelsea ni timu ya baba, timu ya mama, timu ya babu na bibi pia ..kwanini mimi niwe tofauti nao? Hahaha unataka nipate laana mkuu..

Anyway shukrani mkuu.
 
Naona huu mjadala watu wanaufanya kishabiki, imekuwa ligi Kati ya walioajiriwa vs waliojiajiri
Mtoa mada alikuwa na lengo zuri tu Wala sio kuwakatisha tamaa watu kujiajiri, Ni kuwa kujiajiri hasa pale mwanzo sio kitu rahisi Kama unataka kukua kimaisha kweli

Faida kubwa ya kujiajiri kunakupa nafasi ya kujikuza we mwenyewe kadri uwezavyo badala ya kumtegemea bosi afurahishwe na wewe akupandishe cheo na kujipangia ratiba zako mwenyewe

Lakini hili linakuja na price yake pia, hasa pale mwanzo unatakiwa uwe na nidhamu kubwa ili kukuza huo mradi wako na kujijengea reputation nzuri kwa wateja wako (brand)

Kuajiriwa pia sio vibaya unaweza kupata kazi nzuri inayolipa vizuri na ukawa unakua kikazi na kipato pia, lakini hata hili linahitaji nidhamu pia
Lakini kwa sababu kuajiriwa kunakuwa na misingi tayari iliyowekwa na mwenye hiyo taasisi, aliyeajiriwa hana kazi kubwa sana, yeye ni kuendeleza tu pale palipofikiwa na hiyo taasisi iliyomuajiri
Tofauti na anayeanza from scratch kujiajiri mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…