Wakati huu maeneo mengi yanavuna mpunga, na tayari mchele mpya umeisha anza kuuzwa, kwa yule kijana mwenye uchu na mafanikio ni wakati wa kutengeneza pesa tena kwa mtaji kidogo.
Biashara ya mchele ni biashara ya nzuri na hasara zake ni ndogo kutokana na ukweli kwamba huvunwa nchini kwa muda mmoja, yaani kule Morogoro, mbeya na huku kanda ya Ziwa wote huvuna kwa wakati mmoja, sio kama Mahindi ambayo huvunwa mida tofauti na hivyo kufanya soko lisieleweke mfano huku kanda ya Ziwa wanaweza ukanunua mzigo baadae wanavuna Mbeya na kuharibu soko maana bei hushuka.
Ili ufanye biashara ya mpunga wakati inakubidi kwanza ujue aina za mpunga na ubora wake, baada ya hapo tafuta eneo ambalo lina Mavuno mengi na muingiliano mzuri yaani wafanyabiashara hufika kuchukua mzigo, tafuta mtu wa kuuzia mzigo yaani pindi utakapo koboa mpunga wako na kupata mchele uwe na mtu ambae utamuuzia huo mchele, hapa kuna wale wenye mastore.
Baada ya anza kuzunguka kwenye minada (kwa huku kanda ya ziwa) unanunua mpunga unakoboa unaenda kuuza mchele kwa wenye store.
Kama uko serious na kazi kwa ndani ya msimu utakuwa umetengeneza faida mathalani kwa kila gunia la mpunga uwe unapata faida ya shilingi 5,000/= na kwa siku uuze hata gunia 5 za mchele sawa gunia 10 mpunga maanake utakuwa unatengeneza faida ya shilingi 30,000/=~50,000/=.
Jambo la msingi ni kujitoa na kujua thamani ya muda wako, jua mbegu nzuri na jenga uaminifu kwa watu, kwa mtaji mdogo wa 1,000,000/=utakupa faida kubwa.