Vijana ni wakati wa kupiga pesa kwenye biashara ya mpunga

Mi nauza mihogo ya kukaanga kila siku napata faida ya buku tano . Mtaji elfu 30 tu tena Mihogo nanunua buguruni nauli kwenda na kurudi buku vitunguu buku 2 nyanya buku 2 pilipili 500!!.. faida haishuki chini ya buku5!!.. sina swaga kabisa na mbwembwe za mtaji wa milioni 5!.. nanunua kila siku na nauza kila siku na namaliza nyie hangaikeni tu na akili zenu mbovu za kulala porini na kuumwa na mbu mwisho wa siku unapata hasara ya buku kumi kila gunia wakati mi sijawahi kupata hasara...
Kila mtu kuna namna anavyowaza mafanikio usitukatishe tamaa
 
Kama umefanya miaka 3 na hujaacha basi hiyo biashara inalipa, nije kwenye mchanganuo wako kwamba upate faida ya 150, 000/=kila trip ndani ya siku kumi, hivyo basi kwa mwezi utaenda trip 3 mpaka 5 kutegemea na ushapu wako. Kwa mtaji wa million 1 kupata faida ya laki 3 kwa mwezi sio haba.
Vijana twendeni pori.
Porini nenda peke yako mkuu unataka nan akachafuke na kuwashwa na mipunga uko kwa ela ndg iyo ambayo ata konda wa daladala anapata zaidi ya hiyo hahahah
 
Nilichojifunza kuna changamoto nyingi sana ktk kutafuta wapendwa, mfano mi nililima Mara ya kwanza hasara niliyoipata staweza sahau, lakini sikukata tamaaa na niliamni siku nitatoka, ni kweli nililima tena saivi nachekelee nafurahia ukulima Wang, kikubwa usiogope changamoto we pambana ipo siku utatoboza
 
Nimefanya biashara ya mpunga kwa miaka mitatu sasa, Hasara zipo usiseme hasara ni kidogo usidanganye watu kama kusingekuwa na hasara basi wafanyabiashara wote wangenunua mpunga na kuuza Mchele, umesema uuze Gunia 5 kila siku kivipi??? Mpunga unalimwa vijijini interior huko vijini mbali sana naxsehemu za mashine kubwa na wateja, kwa hiyo. 1M kwa bei ya Elf50 mfano, utanunua gunia 20 hizo gunia waweza zikusanya kwa siku 2,3 au hata 4, una gunia 20 hakuna Fuso itakayokufuata kijijini kukupeleka mjini gunia 20 itakubidi ukae huko pori usubiri wenye mitaji mikubwa wapate mzigo ili na wewe wakubebee hizo gunia zako 20 hapo utakaa tena siku zisizopungua 2, ni siku 5 au 6 tayari unafika town kwenye machine hujaanika huo mpunga wako siku 1 au ili ufae kukobolewa then upange foleni ya kukoboa, upige test utafute mteja ndo ukoboe, hivyo kwa trip 1 lazima utumie Siku 10, hivyo kwa mwezi mzima utaenda pori Mara 2 pekee, unakuja kupiga hesabu kila gunia moja ukitoa gharama zote unapata elf 10 au wakati mwingine ukutane na biliani unapata faida ya Elf5, hivyo kwa gunia zako 20 unapata faida ya 150,000 ukienda Mara 2 ndo utaipata Laki 3, kwa mwezi mmoja, hivyo Hii biashara siyo nyepesi na uwe mwanamme kweli siyo mla chipsi, maana unaenda pori week 2 unalala kwenye carpet lile lile mnaloanikia mpunga mchana, kulalia mifuko ya kupimia mpunga na chakula cha kijijini viazi na mihogo uwe umejiandaa kisaikolojia, maana kupata ukurutu ni kitu cha kawaida tu,, Biashara inalipa lakini Mara nyingi kwa wenye mitaji mikubwa, yule anayejaza fuso pekee ake gunia 100 ndo anapata faida maana akijaza mzigo siku hiyo hiyo anapiga simu na kutoka pori wewe wa gunia 10,20,30 unabaki huko.
Mkuu umefafanua vyedu mm nimekuelewa nazani hapo chamsingi nikuanza namtaji wagunia 100 wakujaza fuso
 
Ukiwa na hiyo pesa utakutana na watu wanakuambia bira uwe na pesa ya fuso mbili ndio utaiona faida wewe anza na mtaji wowote ulio nao hata ukiwa na fiada ndogo ni ya kwako utakuwa tu, vijana wa kitanzania hiyo milioni 60 tunatoa wapi
 
Kama umefanya miaka 3 na hujaacha basi hiyo biashara inalipa, nije kwenye mchanganuo wako kwamba upate faida ya 150, 000/=kila trip ndani ya siku kumi, hivyo basi kwa mwezi utaenda trip 3 mpaka 5 kutegemea na ushapu wako. Kwa mtaji wa million 1 kupata faida ya laki 3 kwa mwezi sio haba.
Vijana twendeni pori.
Ngoja tukachukue mitaji finka
 
Rudia nilichoandika sijasema hakuna faida nimesema siyo Rahisi kama ulivyoandika wewe, yaani kama kuweka 1m kwa msimu utapata 10M, hicho kitu hakipo waeleze hatua kwa hatua faida zinapatikanaje na changamoto zake zikoje MTU asije soma bandiko lako na kwenda kuchukua mkopo aje kwenye hii biashara, pointi yangu angalau ukitaka kupata faida Uwe na 5M ndo utaiona faida, pili usiniongelee mimi nimefanya biashara miaka3 hivyo kuna faida, hujui kwamba bado nafanya hiyo Biashara au Hapana, pili hujui Mimi Nilikuwa na mtaji kiasi gani, pili hujui Mimi nilikuwa nanunua na kukoboa na kuuza kila trip na kurudi pori au nilikuwa nanunua gunia 200 naweka store nakuja kukoboa Mara 1 kwa msimu, hivyo Achana na kuni judge mimi, nimetoa ushauri kwa uzoefu wangu Ili MTU Aingie kwenye biashara Akitegemea na Hasara pia, msiwaaminishe tu watu raha na faida tu, changamoto pia waambieni.
Ture point
 
Vip kuhusu kununu mpunga afu unauweka na kuja kukoboa na kuuza mchele msimu ambao mchele umepanda bei?
 
Umenichekesha
Mkuu uyu mleta mada alidharau idea yangu ya biashara akaiita ya kitoto nikajua labda analeta mzigo kutoka china na dubai. Kumbe anahangaika maporoni analalia magunia ili tu akatafute mipunga ! Usitukane watu wakat unaish kwenye nyumba ya vioo. Kila la kheri huko poroni kwenye kusaka mipunga.
 
Kama umefanya miaka 3 na hujaacha basi hiyo biashara inalipa, nije kwenye mchanganuo wako kwamba upate faida ya 150, 000/=kila trip ndani ya siku kumi, hivyo basi kwa mwezi utaenda trip 3 mpaka 5 kutegemea na ushapu wako. Kwa mtaji wa million 1 kupata faida ya laki 3 kwa mwezi sio haba.
Vijana twendeni pori.
Mkuu kumbuka hiyo laki tatu hujatoa matumizi na bado kama umepanga bado kodi
 
Nimefanya biashara ya mpunga kwa miaka mitatu sasa, Hasara zipo usiseme hasara ni kidogo usidanganye watu kama kusingekuwa na hasara basi wafanyabiashara wote wangenunua mpunga na kuuza Mchele, umesema uuze Gunia 5 kila siku kivipi??? Mpunga unalimwa vijijini interior huko vijini mbali sana naxsehemu za mashine kubwa na wateja, kwa hiyo. 1M kwa bei ya Elf50 mfano, utanunua gunia 20 hizo gunia waweza zikusanya kwa siku 2,3 au hata 4, una gunia 20 hakuna Fuso itakayokufuata kijijini kukupeleka mjini gunia 20 itakubidi ukae huko pori usubiri wenye mitaji mikubwa wapate mzigo ili na wewe wakubebee hizo gunia zako 20 hapo utakaa tena siku zisizopungua 2, ni siku 5 au 6 tayari unafika town kwenye machine hujaanika huo mpunga wako siku 1 au ili ufae kukobolewa then upange foleni ya kukoboa, upige test utafute mteja ndo ukoboe, hivyo kwa trip 1 lazima utumie Siku 10, hivyo kwa mwezi mzima utaenda pori Mara 2 pekee, unakuja kupiga hesabu kila gunia moja ukitoa gharama zote unapata elf 10 au wakati mwingine ukutane na biliani unapata faida ya Elf5, hivyo kwa gunia zako 20 unapata faida ya 150,000 ukienda Mara 2 ndo utaipata Laki 3, kwa mwezi mmoja, hivyo Hii biashara siyo nyepesi na uwe mwanamme kweli siyo mla chipsi, maana unaenda pori week 2 unalala kwenye carpet lile lile mnaloanikia mpunga mchana, kulalia mifuko ya kupimia mpunga na chakula cha kijijini viazi na mihogo uwe umejiandaa kisaikolojia, maana kupata ukurutu ni kitu cha kawaida tu,, Biashara inalipa lakini Mara nyingi kwa wenye mitaji mikubwa, yule anayejaza fuso pekee ake gunia 100 ndo anapata faida maana akijaza mzigo siku hiyo hiyo anapiga simu na kutoka pori wewe wa gunia 10,20,30 unabaki huko.

Very true, mie nimeifanya kwa msimu mmoja na changamoto ndo kama alivyosema Swahiba. Yabidi mtu ujipange haswa na uwe na mtaji wa kutosha ili uweze ona faida yake
 
Ni kweli mkuu unahitaji kujipanga haswa, mleta mada sijui aliona nan kapiga ela kwenye mipunga ya maporoni akakurupuka kuja kuhamasisha watu humu waende porini bila hata kufanya upembuzi yakinifu!
 
Habari! Mimi ni kijana natafuta kazii ,vibarua any job iwe halalii tuu nikoo dar, mwenye taarifa yoyote ani Pm
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Back
Top Bottom