Nimefanya biashara ya mpunga kwa miaka mitatu sasa, Hasara zipo usiseme hasara ni kidogo usidanganye watu kama kusingekuwa na hasara basi wafanyabiashara wote wangenunua mpunga na kuuza Mchele, umesema uuze Gunia 5 kila siku kivipi??? Mpunga unalimwa vijijini interior huko vijini mbali sana naxsehemu za mashine kubwa na wateja, kwa hiyo. 1M kwa bei ya Elf50 mfano, utanunua gunia 20 hizo gunia waweza zikusanya kwa siku 2,3 au hata 4, una gunia 20 hakuna Fuso itakayokufuata kijijini kukupeleka mjini gunia 20 itakubidi ukae huko pori usubiri wenye mitaji mikubwa wapate mzigo ili na wewe wakubebee hizo gunia zako 20 hapo utakaa tena siku zisizopungua 2, ni siku 5 au 6 tayari unafika town kwenye machine hujaanika huo mpunga wako siku 1 au ili ufae kukobolewa then upange foleni ya kukoboa, upige test utafute mteja ndo ukoboe, hivyo kwa trip 1 lazima utumie Siku 10, hivyo kwa mwezi mzima utaenda pori Mara 2 pekee, unakuja kupiga hesabu kila gunia moja ukitoa gharama zote unapata elf 10 au wakati mwingine ukutane na biliani unapata faida ya Elf5, hivyo kwa gunia zako 20 unapata faida ya 150,000 ukienda Mara 2 ndo utaipata Laki 3, kwa mwezi mmoja, hivyo Hii biashara siyo nyepesi na uwe mwanamme kweli siyo mla chipsi, maana unaenda pori week 2 unalala kwenye carpet lile lile mnaloanikia mpunga mchana, kulalia mifuko ya kupimia mpunga na chakula cha kijijini viazi na mihogo uwe umejiandaa kisaikolojia, maana kupata ukurutu ni kitu cha kawaida tu,, Biashara inalipa lakini Mara nyingi kwa wenye mitaji mikubwa, yule anayejaza fuso pekee ake gunia 100 ndo anapata faida maana akijaza mzigo siku hiyo hiyo anapiga simu na kutoka pori wewe wa gunia 10,20,30 unabaki huko.