Vijana ni wakati wa kupiga pesa kwenye biashara ya mpunga

Kwanini ulale kwenye Tutubai wakati unaweza nunua sleeping bag ukaenda nalo?,

kwanini ule mihogo daily,wakati unaweza kwenda na ready to eat meal,ukawa unapasha moto kwenye microwave.......ooh wait...
 
Biashara ya mazao ya msimu yahtaji moyo vinginevyo hela italala store na bei haipandi
Umeongea pointi ya msingi sana, watu mwaka Jana tumenunua mahindi gunia Elf 50 tukitarajia kama mwaka juzi kuuza Elf 70-100k now Tumelazimika kuuza mahindi kwa Elf40 Kwa Gunia, hasara ya Elf10 kila gunia ongeza na gharama za kutunza. Hapo umekula hasara ya Elf 20 kila gunia piga hesabu ulikuwa na gunia 100×20,000= hasara ya 2,000,000, 2M kama mwaka Jana mtaji ulikuwa 5M now ukiuza unapata 3M halafu unakuja kusema biashara ya Nafaka ni ya kukurupukia??? Labda kwa yule ambaye hayajawahi ifanya.
 
Mkuu kwa uzoefu wako wa hii biashara kati ya kununua mpunga mashambani na kuja kuuza machineni baada ya kuukoboa na kununua machine kuja kuwauzia akina mangi madukani ipi risk yake ina afadhali
Afadhali kuuza Mchele moja kwa moja.. Pesa yake itachelewa Lakini utaipata yote..
 
Hakuna biashara Rahis niongezee tu kitu kwa jamaa aliesema kafanya miaka mitatu alichoongea ni hakika.

Lakin changamoto nyingine ambayo hamjui ni upimaji wa mpunga we toka tu huko dar uje ujipendekeze pori huku ukadhani hakuna wajanja utapigwa unakuja kusituka muda ushaenda. Kupima mpunga kuna utaalamu wake. Kama hujui waweza kuwa hapo unapimiwa unaona unafika kumbe unaliwa. Iyo Mosi

Pili kujua mpunga mzuri na namna ya kuuandaa kama unaweka store ili kiuza msimu usio mzuri. Walau hili waweza lipa vijana wakaanika badae wakawa wanapiga miguu na wakatupia store. Wafanyakazi biashara siku wanakuja kwanza anaekecha mkononi. Anaona inakatika au inasimama. Then mnakoboa sampo

All in all ukifata procedure na wazoefu waaminifu wakakuongoza. Mungu bariki ukaweka store ukakutana na msimu....ha ha ha utafurai mwenyewe.

Kila la heri kama mnataka mali mtazipata Shambani
 
Kuna mpumbavu hayajui haya atasimama tena na kusema unakatisha watu tamaa
 
Kwanini ulale kwenye Tutubai wakati unaweza nunua sleeping bag ukaenda nalo?,

kwanini ule mihogo daily,wakati unaweza kwenda na ready to eat meal,ukawa unapasha moto kwenye microwave.......ooh wait...
Boss microwave ipi unayowezakitumia ukiwa huko porini kusiko na umeme? Nakuunga mkono kwenye sleeping bag
 
Hiyo biashara ya kutunza mzigo ni biashara ya kimaskini, inazuia mzunguko wa pesa, ni bora upate faida ndogo lakini uwe umezungusha pesa, mathalani baadala ya kutunza ungeyauza kwa faida ndogo, una chukua mengine unauza tena, ungejikuta umepata faida kubwa.

Nina rafiki yangu kama wewe, yeye alinunua Mahindi mengi akaweka ndani mimi nikawa nanunua nauza kwa faida ndogo, mwisho wa msimu nilikuwa nimetengeneza faida kubwa, yeye akala hasara.
 
Mi nauza mihogo ya kukaanga kila siku napata faida ya buku tano . Mtaji elfu 30 tu tena Mihogo nanunua buguruni nauli kwenda na kurudi buku vitunguu buku 2 nyanya buku 2 pilipili 500!!.. faida haishuki chini ya buku5!!..

Sina swaga kabisa na mbwembwe za mtaji wa milioni 5!.. nanunua kila siku na nauza kila siku na namaliza nyie hangaikeni tu na akili zenu mbovu za kulala porini na kuumwa na mbu mwisho wa siku unapata hasara ya buku kumi kila gunia wakati mi sijawahi kupata hasara...
 
Kama hautaweza kufikiria jambo kwa miaka 50 ijayo kuna uwezekano mkubwa ukafa maskini, ndo wale wazee walikua kariakoo enzi hizo kimara ni mapori na hawakununua viwanja.
 
Na wenzako hio buku 5 yako ya faida ya siku wananywea bia 2 tu imeisha.
 
Aisee
 
Ukweli wa mambo ni kwamba hamna kazi nyepesi, kila penye riziki kuna changamoto zake na lazima ujifunze kukabiliana nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…