sizonjemadawa
JF-Expert Member
- Feb 11, 2017
- 1,053
- 1,304
Mkuu naomba nikuulizeVery true, mie nimeifanya kwa msimu mmoja na changamoto ndo kama alivyosema Swahiba. Yabidi mtu ujipange haswa na uwe na mtaji wa kutosha ili uweze ona faida yake
Mkuu naomba nikuulize
Mimi nataka niifanye hii biashara kati ya kununua mchele uliokobilewa na kununua mpunga alafu niukoboe mwenyewe ni kipi kina afadhali kwa sisi wenye mitaji ya m1
Wewe jamaa wewe microwave porini..kazi ipoKwanini ulale kwenye Tutubai wakati unaweza nunua sleeping bag ukaenda nalo?,
kwanini ule mihogo daily,wakati unaweza kwenda na ready to eat meal,ukawa unapasha moto kwenye microwave.......ooh wait...
..Kwa uzoefu mdogo nilionao mpaka sasa na kwa capital hiyo, nadhan ununue mchele kwenye machine kwa sababu kwa mchele angalau unaweza kuona ubora wake (rangi, unyoofu-kwa maana utaona haujakatikakatika). Lakini kununua mpunga ambao utakuletea mchele bora inahitaji uzoefu na utaalam sana. Pia ubora wa mchele hutegemea pia matunzo wakati mpunga tangu ukiwa shambani, muda uliovunwa na hata storage baada ya kuvunwa
TrueJamani msikurupuke kama nguruwe pori aliyekurupushwa kwenye shamba la muhogo fanya walau abc zifuatazo.
Kwanza fanya market research Je kule unapotaka kupeleka huo mpunga/mchele kuna mahitaji makubwa? tani ngapi? je uhitaji huo unasababishwa ni nini? Je waliokua wanapeleka wameishia wapi? Je bei ikoje? aina gani inapendwa?
Pili fanya utafiti kuhusu wapi unaptikana huo mpunga? kwa bei gani? je aina hiyo ndio inapendwa sokoni? je gharama za kununua maka kufika sokkoni ni kiasi gani? what will be your competitive advantage?
Tatu: ikitokea vinginevyo (worse case scenario) unaweza kuhifadhi usubirie soko likae vizuri ama una njia zingine za kurudisha gharama zako?
Mwisho wajue vizuri washindani wako kina nani, wana nguvu kiasi gani, wanawezaje kuwa tishio kwako.
Ukishajipima huko kote nenda kafanye biashara ukiwa unafahamu mazingira yanayokuzunguka
Broo we acha tu, wa tz nomaKwanini ulale kwenye Tutubai wakati unaweza nunua sleeping bag ukaenda nalo?,
kwanini ule mihogo daily,wakati unaweza kwenda na ready to eat meal,ukawa unapasha moto kwenye microwave.......ooh wait...
Zipo microwave za sola jamaniBoss microwave ipi unayowezakitumia ukiwa huko porini kusiko na umeme? Nakuunga mkono kwenye sleeping bag
we jamaa bhana...hv microwave yaweza kufanya kaz bila umeme?? unajua mzngira wanakolima mpunga ww??Kwanini ulale kwenye Tutubai wakati unaweza nunua sleeping bag ukaenda nalo?,
kwanini ule mihogo daily,wakati unaweza kwenda na ready to eat meal,ukawa unapasha moto kwenye microwave.......ooh wait...
hv mda wa kubebelea microwave unaupata wapi?? na hyo sola utakuwa unabebelea kika unapohama shamba?Zipo microwave za sola jamani
Naelewa sasa..Kwa uzoefu mdogo nilionao mpaka sasa na kwa capital hiyo, nadhan ununue mchele kwenye machine kwa sababu kwa mchele angalau unaweza kuona ubora wake (rangi, unyoofu-kwa maana utaona haujakatikakatika). Lakini kununua mpunga ambao utakuletea mchele bora inahitaji uzoefu na utaalam sana. Pia ubora wa mchele hutegemea pia matunzo wakati mpunga tangu ukiwa shambani, muda uliovunwa na hata storage baada ya kuvunwa
Nimefanya biashara ya mpunga kwa miaka mitatu sasa, Hasara zipo usiseme hasara ni kidogo usidanganye watu kama kusingekuwa na hasara basi wafanyabiashara wote wangenunua mpunga na kuuza Mchele, umesema uuze Gunia 5 kila siku kivipi??? Mpunga unalimwa vijijini interior huko vijini mbali sana naxsehemu za mashine kubwa na wateja, kwa hiyo. 1M kwa bei ya Elf50 mfano, utanunua gunia 20 hizo gunia waweza zikusanya kwa siku 2,3 au hata 4, una gunia 20 hakuna Fuso itakayokufuata kijijini kukupeleka mjini gunia 20 itakubidi ukae huko pori usubiri wenye mitaji mikubwa wapate mzigo ili na wewe wakubebee hizo gunia zako 20 hapo utakaa tena siku zisizopungua 2, ni siku 5 au 6 tayari unafika town kwenye machine hujaanika huo mpunga wako siku 1 au ili ufae kukobolewa then upange foleni ya kukoboa, upige test utafute mteja ndo ukoboe, hivyo kwa trip 1 lazima utumie Siku 10, hivyo kwa mwezi mzima utaenda pori Mara 2 pekee, unakuja kupiga hesabu kila gunia moja ukitoa gharama zote unapata elf 10 au wakati mwingine ukutane na biliani unapata faida ya Elf5, hivyo kwa gunia zako 20 unapata faida ya 150,000 ukienda Mara 2 ndo utaipata Laki 3, kwa mwezi mmoja, hivyo Hii biashara siyo nyepesi na uwe mwanamme kweli siyo mla chipsi, maana unaenda pori week 2 unalala kwenye carpet lile lile mnaloanikia mpunga mchana, kulalia mifuko ya kupimia mpunga na chakula cha kijijini viazi na mihogo uwe umejiandaa kisaikolojia, maana kupata ukurutu ni kitu cha kawaida tu,, Biashara inalipa lakini Mara nyingi kwa wenye mitaji mikubwa, yule anayejaza fuso pekee ake gunia 100 ndo anapata faida maana akijaza mzigo siku hiyo hiyo anapiga simu na kutoka pori wewe wa gunia 10,20,30 unabaki huko.
Akili ya kitoto hii.Kama hautaweza kufikiria jambo kwa miaka 50 ijayo kuna uwezekano mkubwa ukafa maskini, ndo wale wazee walikua kariakoo enzi hizo kimara ni mapori na hawakununua viwanja.
Wanapimaje boss tuelimishe tusije kupigwa za usoHakuna biashara Rahis niongezee tu kitu kwa jamaa aliesema kafanya miaka mitatu alichoongea ni hakika.
Lakin changamoto nyingine ambayo hamjui ni upimaji wa mpunga we toka tu huko dar uje ujipendekeze pori huku ukadhani hakuna wajanja utapigwa unakuja kusituka muda ushaenda. Kupima mpunga kuna utaalamu wake. Kama hujui waweza kuwa hapo unapimiwa unaona unafika kumbe unaliwa. Iyo Mosi
Pili kujua mpunga mzuri na namna ya kuuandaa kama unaweka store ili kiuza msimu usio mzuri. Walau hili waweza lipa vijana wakaanika badae wakawa wanapiga miguu na wakatupia store. Wafanyakazi biashara siku wanakuja kwanza anaekecha mkononi. Anaona inakatika au inasimama. Then mnakoboa sampo
All in all ukifata procedure na wazoefu waaminifu wakakuongoza. Mungu bariki ukaweka store ukakutana na msimu....ha ha ha utafurai mwenyewe.
Kila la heri kama mnataka mali mtazipata Shambani
atakulipisha kiingilioMkuu ungetupa mchanganuo wa hiyo million moja katika kilimo cha mpunga
pia muulize ameshajenga/fungua viwanda vingapi toka 2016?Akili ya kitoto hii.
Nikuulize we una hekari ngapi dodoma mjini na ulinunua kabla ya dodoma haijawa jiji?
Wanapimaje boss tuelimishe tusije kupigwa za uso