Katika umri wangu huu,wa miaka kadhaa nimethibitisha pasina shaka Mwanamke hapendi,bali Mwanaume ndio anapenda.
99% ya Wanawake wanaolewa na Wanaume walio tayari kuanza maisha ya ndoa.Mwanamke ataanza kuvutiwa na wewe namna utavyoanza Ku mu care.
Hayo mambo ya Wanawake kupenda mnayaleta nyie Wanaume wa kizazi hiki,ambapo haina justification yoyote.Issue kuu ni maadili-ndugu zetu waarabu wanawake wanachaguliwa Wanaume kama ilivyokuwa zamani huku Afrika but ndoa zao huzisikii zina makando kando mengi maana wanawake wamelelwa katika maadili na wanajua wajibu wao.
Hakuna kiumbe Chenye utashi ambacho kitakosa kitu kinaitwa upendo.
Elewa pia kwenye mapenzi, Mwanamke hawezi kukutii kama Hakupendi.
Mwisho kabisa, Wanawake WA zamani walifanyiwa ukatili ndio maana walichaguliaa wanaume wa kuwaoa.
Na Wazazi waliofanya hivyo wengi wao ni wabinafsi na wajinga kupitiliza.
Swali pekee ambalo mzazi atamuuliza Binti yake Wakati anaolewa ni "unauhakika unampenda kijana huyu/yule?" Lakini wazazi wabinafsi na majinga ndio yanaangalia tuu Mali na mwishowe huenda kuwatesa Binti zao.
Mwanamke anapenda, ingawaje upendo wake haufanani na upendo wa Sisi wanaume. Kama vile ilivyo, Sisi wanaume tunapenda lakini upendo wetu haufanani na Wanawake.
Haki, upendo, ukweli na AKILI. Binadamu atahitaji mambo hayo ili aweze kuishi Kwa Raha. Na Mwanamke pia ni binadamu.
Ni ninyi mnaoishi katika Zama za kale mnaodanganyana na kujifanya hamuwaelewi Wanawake kumbe mnawatafsiri Kwa namna isiyofaa, mliyoikuta, au mlioamua kuchagua.
Zamani mlisema Mwanamke hawezi kuwa Daktari, sasa wapo kibao, zamani mlisema Mwanamke hawezi kuongoza familia, sasa hivi wapo kibao wanaoongoza Familia na hata makampuni makubwa.
Unapomjadili Mwanamke Jambo la Kwanza ni kuelewa kuwa ni binadamu/MTU kama alivyo mwanaume.
Ingawaje tofauti chache zipo.