Championship
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,500
- 10,616
Nimefurahi sana nilipokutana na jamaa zangu tulimaliza chuo mwaka mmoja na wamefanikiwa kimaisha japo hawakuwahi kuajiriwa
Mmoja aliamua kuwa bodaboda pamoja na digrii yake. Kwasasa amejenga nyumba mbeya mjini. Anazo bajaji kadhaa kaajiri vijana na analo duka kubwa la jumla.
Mwingine yeye alizama sokoni kule mafinga na sasa hivi ana duka kubwa sana la vitenge na anao mjengo wa maana sana pale. Watoto wake anasomesha shule kali za Moshi na Dar es salaam.
Mwingine alianza na duka dogo la mangi ambalo lilifilisika. Akapata mkopo kwa ndugu akawa anauza mayai kwenye kibanda. Alipolipa deni akaanza kiduka cha hardware. Leo hii ni supplier mkubwa wa vifaa vya ujenzi.
Ukisikiliza hustling walizopitia sio kitoto. Wamepambana kiume haswa na sasa hivi wameona nuru. Hawa wote wamefight kwa takribani miaka 15 sasa.