Vijana sahauni kuhusu ajira, wenzenu wanafanikiwa kwenye biashara mbalimbali

Vijana sahauni kuhusu ajira, wenzenu wanafanikiwa kwenye biashara mbalimbali

Nilikuwa nakusubiri hapo tu. Mkuu vijana uliowataja kwenye uzi wako hawana uwezo wa kusomesha hizo shule kidooogo labda feza. Nje ya hapo labda green acres,mbezi beach,st.marry's ambapo kwa sasa hizo shule ni bora za serikali au shule yangu pendwa tegeta zamani kwa sasa ni mzumbe university
Mkuu unajidanganya, nawafahamu mpaka wafanyabiashara wanaosomesha watoto wao UK na Marekani kwa kutegemea hizi biashara unazoweza kuzidharau.

Mfano huyo jamaa ambaye ni supplier wa vifaa vya ujenzi kwa sasa mtaji wake upo kwenye bilioni 4+. Yaani ni tajiri kinoma, amejenga mjengo wake pale wilayani ni mzuri kuliko nyumba yoyote iliyopo pale.
 
Nimefurahi sana nilipokutana na jamaa zangu tulimaliza chuo mwaka mmoja na wamefanikiwa kimaisha japo hawakuwahi kuajiriwa

Mmoja aliamua kuwa bodaboda pamoja na digrii yake. Kwasasa amejenga nyumba mbeya mjini. Anazo bajaji kadhaa kaajiri vijana na analo duka kubwa la jumla.

Mwingine yeye alizama sokoni kule mafinga na sasa hivi ana duka kubwa sana la vitenge na anao mjengo wa maana sana pale. Watoto wake anasomesha shule kali za Moshi na Dar es salaam.

Mwingine alianza na duka dogo la mangi ambalo lilifilisika. Akapata mkopo kwa ndugu akawa anauza mayai kwenye kibanda. Alipolipa deni akaanza kiduka cha hardware. Leo hii ni supplier mkubwa wa vifaa vya ujenzi.

Ukisikiliza hustling walizopitia sio kitoto. Wamepambana kiume haswa na sasa hivi wameona nuru. Hawa wote wamefight kwa takribani miaka 15 sasa.

Hongera kwao na congrats wale wote ambao wametoka kwa hustling, lakin kuna dark part ambayo hujaisema.

Si wote wanao pita hiyo path wanafanikiwa
 
Back
Top Bottom