Vijana sahauni kuhusu ajira, wenzenu wanafanikiwa kwenye biashara mbalimbali

Vijana sahauni kuhusu ajira, wenzenu wanafanikiwa kwenye biashara mbalimbali

Yaani hapo unamaanisha utapigq nae stori tu.mbona haujamuomba msingi wa biashara unadhani maneno matupu yatakusaidia kufanikiwa?
Umekataa mfano wa rich dad poor dad?

Au hujaelewa?

Huo ni mfano bora wa kujibu unalouliza, kama ataamua kukuelekeza anaweza akakuulekeza na usijue upo unaelekezwa.

Pointi Hakuna mtu ambaye hajifunzi mkuu.
Au kuelekezwa wewe umeleta masuala ya kujilinganisha off point.

Uzi ulikuwa kama inspirational tu.
 
Nimefurahi sana nilipokutana na jamaa zangu tulimaliza chuo mwaka mmoja na wamefanikiwa kimaisha japo hawakuwahi kuajiriwa

Mmoja aliamua kuwa bodaboda pamoja na digrii yake. Kwasasa amejenga nyumba mbeya mjini. Anazo bajaji kadhaa kaajiri vijana na analo duka kubwa la jumla.

Mwingine yeye alizama sokoni kule mafinga na sasa hivi ana duka kubwa sana la vitenge na anao mjengo wa maana sana pale. Watoto wake anasomesha shule kali za Moshi na Dar es salaam.

Mwingine alianza na duka dogo la mangi ambalo lilifilisika. Akapata mkopo kwa ndugu akawa anauza mayai kwenye kibanda. Alipolipa deni akaanza kiduka cha hardware. Leo hii ni supplier mkubwa wa vifaa vya ujenzi.

Ukisikiliza hustling walizopitia sio kitoto. Wamepambana kiume haswa na sasa hivi wameona nuru. Hawa wote wamefight kwa takribani miaka 15 sasa.
Dah kwa umri nilionao nikisema nifaiti miaka 15 huenda nikatoboa nikiwa hata "bone marrow" hausimami kabisa.
 
Kufanikiwa katika maisha sio lazima wote tusote, wengine msote na wengine tujifunze kupitia misoto yenu, running a business into success sio kazi rahisi na sio kila mtu anaweza sometimes ni akili ya ziada itumike kufanya biashara ikue na ifanikiwe,
Mafanikio yanayodumu yanahusisha kufanya kazi kwa akili na bidii. Kuna kazi mtu mmoja anaweza kuiona ni ya kusota wakati mtu mwingine anaweza kuiona ni ya kawaida. Cha muhimu ni kupambana kufikia maono na ndoto tulizonazo.
 
Umeshauri vizuri lakini ulivosema anasomesha shule kali dar es salaam ndo nimechoka. Huwenda hata hii ni stori yà kufikirika tu
Kwanini umechoka kusema shule kali DSM?
Umemuelewa kuhusu shule kali?
 
Waarabu,wahindi na wakinga walipoona kusoma ni kupoteza pesa na mda mliwaona wajinga mmelewa kwa kuchelewa wao toka kitambo miaka 40 nyuma waliona upumbavu.
Wakati we unakesha kukariri akimedesi principal ili ushinde mtihani wao wanasaka life experience kwa kupokea Hela au kutoa chenji,kufuta vumbi store,clutch ipo wapi,
We Hadi umalize chuo ndo uje uitumie hizo unapplicable principle utasaga sana sori kujaribu kuokota ajira utafika 40 hata mtoto wa dawa huna huku mwenzako mtoto wake yupo chuo,
 
Pointi yako ni ipi sasa ndugu bongo dili?
 
Pointi yako ni ipi sasa ndugu bongo dili?
Soma mwisho form four ili ukue na kuondoa kelele nyumbani,jioni baada ya shule jichanganye mtaani fanya hobby yake.
Ulimwengu umebadilika hautaki vyeti bali ujuzi wa kuchukua pesa toka kwa watu.
Utachukuaje pesa kwa watu kama huna ujuzi.
Ujuzi ni kujua watu wanataka Nini mbadilishane wakupe pesa zao.
 
sawa tuseme nakubaliana na wewe tusome wote mwisho form four.

Nani ataenda kukutibia wewe pale muhimbili wote tukisoma mwisho fom4?

Umefikiria upande wa pili wa shilingi?
 
Kila tajiri ana historia yake ya kutajirika ambayo haifanani na mtu yoyote.na kila tajiri ana siri yake ya utajiri ambayo haifanani na mtu yoyote.kwanini sitaki kumuangalia mtu.ni kwa sababu nitajiona NIMECHELEWA.nitajiona nimepoteza,nitajiona sina maana,nitajiona nimefeli n.k.
Yaani nikikuona wewe unaendesha gari wakati mimi natembea kwa miguu lazma nitajihisi kufeli nitakapotaka kujilinganisha na wewe.
Principle za utajiri ni zile zile tangu zama za selemani.
Mojawapo ni kujituma
Uvumilivu nk
 
Back
Top Bottom