passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,828
- 3,922
Umekataa mfano wa rich dad poor dad?Yaani hapo unamaanisha utapigq nae stori tu.mbona haujamuomba msingi wa biashara unadhani maneno matupu yatakusaidia kufanikiwa?
Dah kwa umri nilionao nikisema nifaiti miaka 15 huenda nikatoboa nikiwa hata "bone marrow" hausimami kabisa.Nimefurahi sana nilipokutana na jamaa zangu tulimaliza chuo mwaka mmoja na wamefanikiwa kimaisha japo hawakuwahi kuajiriwa
Mmoja aliamua kuwa bodaboda pamoja na digrii yake. Kwasasa amejenga nyumba mbeya mjini. Anazo bajaji kadhaa kaajiri vijana na analo duka kubwa la jumla.
Mwingine yeye alizama sokoni kule mafinga na sasa hivi ana duka kubwa sana la vitenge na anao mjengo wa maana sana pale. Watoto wake anasomesha shule kali za Moshi na Dar es salaam.
Mwingine alianza na duka dogo la mangi ambalo lilifilisika. Akapata mkopo kwa ndugu akawa anauza mayai kwenye kibanda. Alipolipa deni akaanza kiduka cha hardware. Leo hii ni supplier mkubwa wa vifaa vya ujenzi.
Ukisikiliza hustling walizopitia sio kitoto. Wamepambana kiume haswa na sasa hivi wameona nuru. Hawa wote wamefight kwa takribani miaka 15 sasa.
usipo ambulia kitu walah utakua na hitilafu ya ubongoNimemuelewa sana.ila na mimi nimeweka kanuni yangu ya maisha.
Labda nikuulize swali ukienda kwa bakhresa utajifunza nini kutoka kwake?
Bahati mbaya hakuna shortcut ya mafanikio yanayodumu. Lazima kupambana.Dah kwa umri nilionao nikisema nifaiti miaka 15 huenda nikatoboa nikiwa hata "bone marrow" hausimami kabisa.
Mafanikio yanayodumu yanahusisha kufanya kazi kwa akili na bidii. Kuna kazi mtu mmoja anaweza kuiona ni ya kusota wakati mtu mwingine anaweza kuiona ni ya kawaida. Cha muhimu ni kupambana kufikia maono na ndoto tulizonazo.Kufanikiwa katika maisha sio lazima wote tusote, wengine msote na wengine tujifunze kupitia misoto yenu, running a business into success sio kazi rahisi na sio kila mtu anaweza sometimes ni akili ya ziada itumike kufanya biashara ikue na ifanikiwe,
hawa wanakuwa kwenye lile kundi la asilimia 16 (laggard) sio early adoptersHakumuelewa mtoa mada, anaongea kitu tofauti.
Unapafahamu dar es salaam au unapasikia? Au unabisha dar hakuna shule nzuri?Umeshauri vizuri lakini ulivosema anasomesha shule kali dar es salaam ndo nimechoka. Huwenda hata hii ni stori yà kufikirika tu
Kwanini umechoka kusema shule kali DSM?Umeshauri vizuri lakini ulivosema anasomesha shule kali dar es salaam ndo nimechoka. Huwenda hata hii ni stori yà kufikirika tu
Pointi yako ni ipi sasa ndugu bongo dili?Waarabu,wahindi na wakinga walipoona kusoma ni kupoteza pesa na mda mliwaona wajinga mmelewa kwa kuchelewa wao toka kitambo miaka 40 nyuma waliona upumbavu.
Wakati we unakesha kukariri akimedesi principal ili ushinde mtihani wao wanasaka life experience kwa kupokea Hela au kutoa chenji,kufuta vumbi store,clutch ipo wapi,
We Hadi umalize chuo ndo uje uitumie hizo unapplicable principle utasaga sana sori kujaribu kuokota ajira utafika 40 hata mtoto wa dawa huna huku mwenzako mtoto wake yupo chuo,
Soma mwisho form four ili ukue na kuondoa kelele nyumbani,jioni baada ya shule jichanganye mtaani fanya hobby yake.Pointi yako ni ipi sasa ndugu bongo dili?
sawa tuseme nakubaliana na wewe tusome wote mwisho form four.Soma mwisho form four ili ukue na kuondoa kelele nyumbani,jioni baada ya shule jichanganye mtaani fanya hobby yake.
Ulimwengu umebadilika hautaki vyeti bali ujuzi wa kuchukua pesa toka kwa watu.
Utachukuaje pesa kwa watu kama huna ujuzi.
Ujuzi ni kujua watu wanataka Nini mbadilishane wakupe pesa zao.
Principle za utajiri ni zile zile tangu zama za selemani.Kila tajiri ana historia yake ya kutajirika ambayo haifanani na mtu yoyote.na kila tajiri ana siri yake ya utajiri ambayo haifanani na mtu yoyote.kwanini sitaki kumuangalia mtu.ni kwa sababu nitajiona NIMECHELEWA.nitajiona nimepoteza,nitajiona sina maana,nitajiona nimefeli n.k.
Yaani nikikuona wewe unaendesha gari wakati mimi natembea kwa miguu lazma nitajihisi kufeli nitakapotaka kujilinganisha na wewe.
Soma huku unajiongeza,maana wote hamuwezi ajiriwa.sawa tuseme nakubaliana na wewe tusome wote mwisho form four.
Nani ataenda kukutibia wewe pale muhimbili wote tukisoma mwisho fom4?
Umefikiria upande wa pili wa shilingi?