Vijana sahauni kuhusu ajira, wenzenu wanafanikiwa kwenye biashara mbalimbali

Na Wewe???
 
Kwahiyo hao wanne ndo wamefanya umekuja na generalization ya kiboya hivyo
 
Upo sahihi lakini nikuhakikishie kuwa haya mambo yanahitaji kutafakari kwa kutumia upeo mkubwa wa akili na siyo kama tunavyofanya. Ni hivi: serikali yetu imeshafeli na nchi sasa hivi ipo inajiendea kama gari lisilo na breki. Nikuulize: hivi vijana wote wasio na ajira wakinunua bodaboda na au wakifungua maduka ni nani atamhudumia mwingine? NI nani atakuwa mteja na nani atakuwa mtua huduma?
 
Hivi hili neno winga ndio dalali.?.Maana kuja nako mjini uzeeni ni kazi😂😂
 
Muwe mnatoa na mifano ya waliofeli pia maana hao ndio wengi, wote tunajua hali ya kujiajiri kwa hapa bongo haina tofauti sana na hali ya kuajiriwa, hii mifano mnayoitoa ya wachache waliofanikiwa haisaidii wala haielezei hali halisi

Hayo ya kusema ukifanya biashara ndio una uhakika wa kuwa millionaire kuliko ukiajiriwa ni huko mbele siyo bongo, huku kuna wafanyabiashara kibao hawatajiriki hadi wanazeeka na kufa, ilihali kuna waajiriwa wanakuwa mamillionaire kupitia ajira zao na usitake kujua wametajirikaje

Hata kwenye ajira nako watakupa mifano ya waliofanikiwa kupitia kuajiriwa kwao
 
Braeburn, IST, Feza, DIA, FK nk
Nilikuwa nakusubiri hapo tu. Mkuu vijana uliowataja kwenye uzi wako hawana uwezo wa kusomesha hizo shule kidooogo labda feza. Nje ya hapo labda green acres,mbezi beach,st.marry's ambapo kwa sasa hizo shule ni bora za serikali au shule yangu pendwa tegeta zamani kwa sasa ni mzumbe university
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…