Vijana someni Uuguzi, una fursa nyingi

Sidhani kama utakuwa sawa ukiogopa kuitwa nurse, mimi ni nurse na ni Me, wala sina tatizo, mbona ni sawa tu kwangu, maana hata avatar yangu inajieleza kabisa?
Hongera Sana
 
Mtoa mada nakuunga mkono, position nilipo naiona hii fursa ya ajira kupitia uuguzi.
 
Kwahyo ww unachoona shida ni kuitwa nurse mbele za watu!!...embu acha ujinga na zama za kale hii ni karne ya 21 mambo kama hayo yaache!
 
Hapa naona watu wanakosoa. Nakumbuka simulizi ya PEPE HUNA MASIKIO
 
sawa mkuu kwahyo ww ni nurse
Zaidi ya Nurse. Nimefanya kazi na medical attendants, nurses wa certificate hadi degree lakini kwa upande wa intern nurses walio wengi sijafurahishwa na competence yao, nurses wa masters nilikutana nao mazingira ya shule tu nao bado ni wachache sana.

Kwa upande wa madaktari nimekaa na COs, MDs, Intern doctors (wengi wao wababaishaji), MDs (hawa wengi wao wako vizuri ila kuna wengine siwezi pekeka mgonjwa wangu kwao), Residents (hawa nawapenda sana si wavivu wanachapa kazi na ndio nimekaa nao mda mrefu zaidi) na Specialists ( hawa sasa ndio madaktari, wengine nawashauri someni japo nanyi mko vizuri)
 
Ukisema hivyo ujue pia Kuna Co's hadi tertiary settings,, hivi ratio ya Dr's na population ikoje chief?
Tertiary setting ipi ina COs? Kwa navyojua Tertiary setting ni kama MNH, BMC, KCMC na MZRH. Kama hizi hospitali za rufaa za kanda zina COs basi tuna balaa kubwa sana katika sekta ya afya. Mimi niliposomea hata wale AMOs hawapo
 
Kumbuka nesi hajui systemic pathology and these is the mainstay in diagnosing diseases...half unavosema nesi anaisoma anatomy kumbuka anatomy ya nesi sio sawa na ya daktari,doctor anasoma hadi dissectional anatomy huku nesi akiishia theory tu...sjui labda n kwa chuo nachosoma mm ila nesi na Dr kuwa sawa utatumia muda sana kuniaminisha
 
Unachoongea inaweza kuwa kweli...market ya udaktari inaweza ikawa ni ndogo kulko ya unesi kwa sababu kuajili docta is very expensive kulko nesi...kumbuka vitu vya bei poa vina walaji wengi sana
 
Asome systemic pathology ili naye awe daktari? Yeye ni nurse ana mambo yake ya kusoma ambayo wewe ukiwa unasoma hiyo pathology yeye anayake mengine anasoma but mwisho wa siku wote mtakutanishwa kwa mgonjwa. Nursing na Medicine ni vitu viwili tofauti
 
Unachoongea inaweza kuwa kweli...market ya udaktari inaweza ikawa ni ndogo kulko ya unesi kwa sababu kuajili docta is very expensive kulko nesi...kumbuka vitu vya bei poa vina walaji wengi sana
Acha kukoment kwa mihemko na pengine u mwanafunzi na kama ni daktari utakuwa clinician tu huna uongozi wowote. Twende kwa topic; Unazungumzia nurse wa level ipi na daktari wa level ipi? Kwa upande wa Nurses kuanzia level ya certificate wanatambulika kama nurses lakini kwa upande wa madaktari ni kuanzia level ya degree wewe ndo angalau kidogo unakuwa daktari.

COs ambao ndio madaktari wenu na Nurses wa diploma ni wa level moja na gharama za kuwaajiri ni zile zile na mishahara wanalingana. Nurse wa degree kwanza ni wachache kuwaajiri nao bado ni gharama japo hazifanani na za madaktari
 
Kama ktk hospital moja wanaajiri wauguzi wengi kuliko madaktari inamaana kuwa hawawezi kulipwa vizuri kuliko MD's.
 
Ulichokisema ni kweli ila hii in fani ya kike. Nawasilisha
Historically na jamii inavyoichukulia lakini kiuhalisia hali ni tofauti siku hizi kwa sababu nyingi lakini kwa leo nakupa hii kwa mfano halisi: Nenda Bugando, Muhimbili, KCMC, UDOM, St John's university kaangalie wanao soma bachelor of Nursing utakuta Me ni wengi kuliko wanawake na kwa vyuo vya Diploma vivyo hivyo. Hii ni kwa sababu entry qualifications zimebana tofauti na zamani ambapo hata ambaye hakusoma PCB alisoma nursing.

Kwa siku hizi kama huna hayo masomo ya sayansi kasomee fani zingine na ndio maana dada zangu wanazidi kupungua huku kwenye uuguzi kwa sababu kama tunavyojua ufaulu wao kwa masomo ya sayansi ni mdogo ukilinganisha na watoto wa kiume
 
Mkuu umeona mbali sana,atakayekuelewa
atafika mbali,kuna msemo unaosema
''Ni wapumbavu tu wasioweza kubadilisha mtazamo wao''
Mwisho wa siku heshima inaletwa na una nini mkononi mwako
na sio ulisomea nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…