Vijana nasisitiza tena na tena, kama wewe unatoka familia maskini ambayo unategemewa upate ajira ili usaidie familia yako course yenye uhakika wa angalau kupata ajira ndani na nje ya Nchi ni Uuguzi. Kama unataka kujiajili mwenye we pharmacy ni ya kwanza na nursing inafuata. Habari za MD ilikuwa zamani hizoooo mama yako hajazaliwa. Hebu fikiria TU muhimbili kila mwaka inazalisha madaktari wapy 300, KCMC 300, Bugando 310, Kairuki 270, UDS 350, Kampala International University 360, UDom 500, na St. John's 400. Hebu nambie hao ni kwa mwaka mmoja TU na kila siku juhudi kwenye vyuo zinafanyika ili kuongeza majengo na walimu ili kuongeza udahili wa wanafunzi hao, na TCU imeshusha ufaulu wa kujiunga na kozi ya MD hadi DDD, Yani D physics, D kemia vna D biology. Ufaulu wa kujiunga na kozi ya nursing chuo kikuu uko juu kuliko ule wa MD, bila kuwa na C ya kemia huwezi kujiunga na Uuguzi. Jamani msidanganywe na historia, fuata trend