Vijana tukumbushane, tusisahau kupima, Kaswende, Kisonono viko nje nje

Vijana tukumbushane, tusisahau kupima, Kaswende, Kisonono viko nje nje

Kuuvuka ujana ukiwa salama ni kumshukuru Mungu kuna sehemu tumepita na tumetoka salama mpaka huamini. Na kuna watu wapo very decent ila mistake moja inapita nao.

#KinganiMuhimu
ndivyo maisha yalivyo, kuna watu ni waaminifu sana ila wanayokutana nayo kwenye mapenzi yanawavuruga jumla, magonjwa ya zinaa hayanaga huruma hata kidogo. Ni mbaya sana kupima kwa macho
 
Mkuu tunahitaji ufafanuzi kuhusu hicho kipimo unatumia damu magonjwa yote hayo au?...au gono na kaswende unakaingiza kwenye k?
Mkuu kioimo ukiweka damu mara moja kinaangalia ukimwi na kaswende.

Ni vipimo vinaitwa dual, vinapatikana famasi ama zahanati.

Ndio vipimo vya kisasa.

Ukienda suka la dawa omba dual utapewa.
 
sasa mbn hakuna haja ya kupima maana unapima kaswende kumbe mtu ana ngoma au unapima ngoma kumbe mwenzio ana kisonono.

utakuwa na vipimo vingapi sasa? ukiwa na vipimo vyote ivo geto linageuka kuwa famasi na wew ndo nesi sijui ndo dokta mwenyew😆
Hicho kipimo kinapima ngoma na kaswende vyote kwa pamoja.
 
Magonjwa ya ngono yanayoua watu wengi. Sio hayo watu wanayoyapima pima

Homa za ini B na C na kansa ya damu, na kansa ya kizazi ndizo zinaua sana watu hapa Tanzania.. zote hizo zinaambukizwa kwa ngono.

Ili watu hawaziongelei.. wanakomaa kupima HIV na hizo gono na kaswende tu
Kansa ya damu inaambukizwa kwa ngono?

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Wiki kama mbili nyuma mwanangu mmoja ambaye ni rafiki wa kitambo sana namjua tabia zake na yeye anajua zangu kwenye kuongea akaingiza stori za madem nikamshauri hawa chura wa mjini piga na kinga tukaongea mengi sana juzi kushinda jana kanifuata tena kwa aibu ananionyesha kashaukwaa ana kaswende na imemla vibaya anamalengelenge makubwa kama matatu ikabidi nicheke kwanza maana kapagawa na kabla hajajua alichovya kwa mkewe kwahyo kuna uwezekano kamuambukiza. Sikutaka kumlaumu kwa alivyochanganyikiwa nikampeleka kwa mshkaji wangu ambaye ni doc akampa dawa na maelekezo sasa kimbembe kinakuja kwa wife wake atakwepaje kutofanya mapenzi kwa muda wa wiki mbili mpka tatu na anaanzaje kumtibu mkewe kama amemuambukiza. Tuwe makini jamani mwenye ugonjwa hajulikani lakini linapokukuta na kama unamke inakua balaa zaididoctor anakuambia hayo malengelenge yatapasuka patakua kidonda na hakiponi mpka zipite wiki mbili na muda mwingine kama unamwili usiopona haraka inaenda mpka wiki tatu na bado litabaki kovu jeupe kwa muda mpka liishe ni zaidi ya mwezi na wiki kadhaa sasa nadhani mnaona changamoto anayokwenda kupitia. Nimeshauriana nae anatabia ya kumpeleka wife wake akakae na mama yake akaona ni idea nzuri mpka apone ila kama kamuambukiza mke sijui huo msala anausolve vipi. Tunapopata bahati ya kukumbushana mambo kama haya tuyazingatie sana hakuna mjuaji kwenye ngono na magonjwa yake
 
Back
Top Bottom