Vijana tunapitia wakati mgumu sana kwenye utafutaji. Chukua hii, itakufikirisha zaidi

Vijana tunapitia wakati mgumu sana kwenye utafutaji. Chukua hii, itakufikirisha zaidi

Kwa sangoma ni big NO kurudi, ni bora nikapambana na mishe zangu tu zinazoniingizia pesa nzuri tu ya kujimwambafai hapa mjini...
Usisahau umeshasajiriwa kule kwa Sangoma kwa hio wewe ni mwanachama hai wa wachawi maana data zako zote wanazo ulishaziacha kule namaanisha kule Gizani bado wanakutambua wewe ni mchawi mwenzao hata km umesitisha kuzitumia dawa zao

Ni km unavyojiunga na Mfuko wa Bima za Afya ukishatibiwa hospital data zako zote zinabaki kwenye database ya Mfuko wa Bima za Afya
 
Aisee umeamua kunipa ukweli mchungu ujue?!
 
Daaah umeandika kwa hisia sana.

Ila kaa ukijua biashara yoyote kama ulivyo fanya hiyo ya mabag huwa kuuza 10 bags per month ni kawaida kwani huwa ni ya msimu so learn how to stay low key na siku ukija msimu wa high peak komaaa kufa kupona uuze bags kama kichaaa maana pesa huwa zinamwagika....

Huwezi kuuza kila siku hata uwe location nzuri...
Uko sahihi asilazimishe biashara ya mabegi tu kila siku,sio kila siku watu wanatumia mabegi na hata mtu akinunua begi hadi lipasuke itachukua miaka miwili.
Angejaribu na biashara ya chakula au vinywaji ambavyo kila binadamu ananunua na anatumia kila siku kisha alete mrejesho tena
 
Soma hadithi yote kisha ujibu upya, hakuna sehemu yoyote nilipoandika nimeng'ang'ana na hiyo biashara
 
Kama ni mkristo nunua ubani ule wa kanisani sio ule wa kuitia maruhani kwa waganga wa kienyeji ni ule ambao mapadri wa kikatoliki uchoma altareni wakati wa misa takatifu ni tabu kidogo kuupata kisha tafuta siku tulivu isiyo na vurugu hasa usiku ni vizuri zaidi uwe msafi kimwili uchome huku ukimuita Mungu, mwambie Mungu mikwamo yako na changamoto zako, Mungu ndiye muumba wa kila kitu duniani anatujua tungali tumboni mwa mama zetu anajua kila pito lako atakuwekea njia pasipo na njia kwasababu njia za Mungu hazichunguziki.

Nakupa mfano: rafiki yangu alipoteza mke na mtoto wakati wa kujifungua muhimbili baada ya maziko mke alimtokea sana mumewe kwenye ndoto za kila wakati akimuita mumewe amfuate alipo, alizunguka kwa waganga kupata dawa lakini wapi siku moja wazo likanijia nikamwambia tafuta ubani wa kanisani choma kisha lalamika kwa Mungu, mwambie tisho lako Mungu ndiye kila kitu ataleta solution, sasa ni mwaka wa kumi na mbili mke hajamtokea tena ndotoni. God knows everything.
 
Kama ni mkristo nunua ubani ule wa kanisani sio ule wa kuitia maruhani kwa waganga ni ule ambao mapadri wa kikatoliki uchoma altareni wakati wa misa takatifu ni tabu kidogo kuupata kisha tafuta siku tulivu isiyo na vurugu hasa usiku ni vizuri zaidi uwe msafi kimwili uchome huku ukimuita Mungu, mwambie Mungu mikwamo yako na changamoto zako, Mungu ndiye muumba wa kila kitu duniani anatujua tungali tumboni mwa mama zetu anajua kila pito lako atakuwekea njia pasipo na njia kwasababu njia za Mungu hazichunguziki.

Nakupa mfano: rafiki yangu alipoteza mke na mtoto wakati wa kujifungua muhimbili baada ya maziko mke alimtokea sana mumewe kwenye ndoto za kila wakati akimuita mumewe amfuate alipo, alizunguka kwa waganga kupata dawa lakini wapi siku moja wazo likanijia nikamwambia tafuta ubani wa kanisani choma kisha lalamika kwa Mungu, mwambie tisho lako Mungu ndiye kila kitu ataleta solution, sasa ni mwaka wa kumi na mbili mke hajamtokea tena ndotoni. God knows everything.
Nitafanyia kazi hili suala
 
Biashara ni lazima uwe vizur kiroho ...

Jifunzen Kwa wahindi,waarabu na wakinga..Kila siku kabla hajaanza biashara kuchoma maudi na ubani...msifikiri anaigiza..wanajua wanachofanya.

Na Kwa sisi wakristo tumieni damu ya Yesu but hakikisha una uhusiano mzuri nae...

Biashara sio lelemama biashara sio ya watu laini laini.. ndio maana wengi wanakimbilia kuajiiriwa.

Biashara ni vitaa kama zilivyo vita zengine za Russia na Ukraine
 
Kabla hujaanza Biashara yako,ita viongozi wa Dini waiweke Wakfu kwa Mungu wako,Kisha toa Zaka na Sadaka,Hakuna Mchawi wala Shetani atakaye gusa hiyo Biashara mana umeikabidhi kwa Mungu.
 
Kabla hujaanza Biashara yako,ita viongozi wa Dini waiweke Wakfu kwa Mungu wako,Kisha toa Zaka na Sadaka,Hakuna Mchawi wala Shetani atakaye gusa hiyo Biashara mana umeikabidhi kwa Mungu.
Mi najuaga wakfu kwenye nyumba na unaandaa chakula vinywaji kidogo, kumbe mpaka biashara.
 
Nipo hapa kwa kitanda usiku huu wa manane nikiwa na msongamano wa mawazo na kutafakari mambo mbalimbali kuhusu haya maisha hasa kwa sisi vijana ambao tunajitafuta na bado hatujajipata.

Haya maisha ya utafutaji yamejaa vitu vigumu na vizito ambavyo siyo rahisi mtu kukuelezea ni namna gani aliweza kufanikiwa katika maisha na kufikia level aliyopo.

Tukubali ama tukatae ila ukweli ni kwamba kila mmoja wetu katika maisha ya utafutaji ana LIGHT SIDE na DARK SIDE yake lakini upande unaomtambulisha mtu hadi akawa midomoni mwa walimwengu kwa kile anachokifanya ni DARK SIDE ambayo inakuwa ni SIRI ya muhusika na tusije danganyana. LIGHT SIDE huwa inatumika kama mfuniko na ngozi ya kuficha nyama ya ndani ambayo ni DARK SIDE.

Muda mwingine unaweza kuamini hiki kumbe sicho na kile usichokiamini ndo ndicho, kinachopaswa kuzingatiwa ni kujua na kuelewa namna ya kutofautisha kipi ni sawa na kipi siyo sawa.

Ilikuwa mwaka 2019 nilijichangachanga nikapata kama 2.5 Milion nikafungua biashara ya duka la chakula(duka la mangi) maeneo fulani hapa jijini Dar es Slaam.

Baada ya kufanya biashara kwa takribani miezi 2, nilianza kutotamani kwenda kufungua hii biashara yangu, yaani ilikuwa kila nikitaka kwenda kazini kunakuwa na kaubaridi jumlisha uoga, miguu kuwaka moto nikiwa maeneo ya biashara, kuchoka na kuumwa ghafla ambao hadi leo hii sijawahi kuelewa shida ilikuwa nini, japo mimi huwa ni muoga na kutoamini sana mambo ya nguvu za giza.

Motokeo yake niliamua kufunga ile biashara kwa kuuza vitu kwa bei ya jumla kwa hasara kubwa mno na baada ya hapo niliamua kuachana na masuala ya biashara nikajikita kwenye mishe zangu zingine.

Mwaka jana baada ya zoezi la Sensa (2022), wazo la biashara lilinijia nikajichangachanga nikafungua biashara ya kuuza mabegi ya mtumba hasa haya ya watoto wa shule na watu wazima hasa wale wa kwenda site i.e kubebea vitu vya mafundi.

Niliamua liwalo na liwe hata iweje ile hali ya kukatia tamaa biashara yangu kama ingenijia, ningekaza na nisingejaribu kukata tamaa.

Nilipambana na hiyo biashara wee japokuwa kuna muda ile hali ilikuwa inanijia lakini nilijikaza kiume. Kuna kipindi mwanzoni mwanzoni kama February mwaka huu (2023) biashara ikawa ngumu kiasi hivyo nikaona nihamishe location ya biashara.

Nilihamia sehemu yenye mzunguko wa watu na biashara ilichangamka sana hadi nikawa nauza hadi 20 bags per day.

Baada ya muda kama miezi 3 toka nihamie hii location mpya, biashara ilianza kuwa ngumu ghafla kwangu, ikawa hata kwa siku naweza uza 1 bag au nisiuze kabisa na mzigo upo wa kutosha. Uvumilivu ulinishinda nikamshirikisha mwanangu mmoja hivi akanielekeza kwa mtaalamu (Sangoma) mmoja huko Mbagala Chamazi ndani ndani.

Ni kweli baada ya mtaalamu mambo yakawa mwororo kama kwa muda wa mwezi mmoja hivi na ghafla mambo yakawa magumu tena balaa. Niliona hata kama uvumilivu wa kibiashara si kwa mtindo huu, yaani majumuisho ya mauzo kwa mwezi ni 10 bags. Niliamua kufunga hii biashara maana sikutaka kuwa mtumwa tena wa kwenda kwa mtaalamu.

Enyi motivation speakers hasa wa masuala ya biashara, mkiwa mnawaponda watu wanaofunga biashara kwa falsafa zenu eti kukosa mitaji, ubunifu na usimamizi mbaya, basi muwe mnakumbuka kuwa kuna masuala ya nguvu za giza na mnapaswa kuyajumlisha kama mojawapo ya changamoto zinazosababisha biashara kufungwa.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

DON YRN.
Mkuu kwanini uliachana na uyo mtaalamu kama hana masharti yanayopingana na misimamo yako.
 
Uko sahihi asilazimishe biashara ya mabegi tu kila siku,sio kila siku watu wanatumia mabegi na hata mtu akinunua begi hadi lipasuke itachukua miaka miwili.
Angejaribu na biashara ya chakula au vinywaji ambavyo kila binadamu ananunua na anatumia kila siku kisha alete mrejesho tena

Yaani kila msimu abadili biashara .
Sio lazima utoe ushauri
 
Back
Top Bottom