Vijana wa 2000 watasema hii ni pakiti ya majani ya chai🤣

Demu Bado upo nae.?
 
Kuber hiyo sijui iliuzwa 300 akati inatoka na viroba vya Zed vikinukia flavor ya pineapple nlitoroka sana shule kuvitafuta akiiii nlikuwa sifai
me nilikuwa nanunua mkanda mzima zilikuwa kama 20 ivi naenda nazo shule (boarding) fizi ziliungua zilibadilika zilikuwa nyeusii wakati nipo likizo home niaharudi chumba kilikutwa kimejaa makiberi tupu niligombezwa sana!
 
Acheni tuu wakuu namlaumu Binamu kunifundisha ila namshukuru kunifundisha kwa kiasi.

Pia Mungu Amrehemu Alikeshi wa Arusha kwa kuileta Kuber Arusha kwa kuwa alijinyonga baadae.

Kuberi Ilikuwa Hatari Sana.
Kww nini alijinyonga mkuu, ilimuharibu kichwa,!?
 
Kuber ukiwa na kichwa mbovu ukiieka mdomoni ukiwa umekaa chini kwa mara ya kwanza hunyenyuki, ukiweza unaweza tembea umeinama ukihofia kugonga nyaya za nguzo za umeme yaan zile nyaya unaziona hizi hapa usoni basi ukizikaribia unainama aisee😀
 
Usinikumbushe mkuu. Miaka ya 90s kuelekea 2000 huo ulevi ulikuwa kama fasheni kwa vijana.

Siku hiyo nikaenda kununua. Mimi na mjomba wangu tukaijaribu. Ebhana weee!!. Kila mtu aliinama kasizi kwenye kona yake kwa kama dakika 30 bila kutikisika. Kichwa kizito, unatamani kukaa na kulala kwa muda mmoja.

Usikute sababu ya kupigwa marufuku kuna viongozi wasiotaka kilevi kiwapite mbele yao wakaijaribu. Nao wakaona mziki wake. Wakaona mhh!!, hii siyo.
 
Kuiona tu hiyo pakti imenifanya kichwa kianze kuniuma kwasababu ni mojawapi ya memory mbaya niliyonayo, ilichonifanya sitasahau.
Nilibwia nyingi na papo hapo nikanywa viroba kipindi hicho vilikuwa maarufu Sana nimesahau jina aisee nashukuru Mungu alininusuru sikukata Moto ila Ile ilikuwa inanipeleka.
SITASAHAU NA TANGU HAPO NILIAPA SITAKUJA KUNYWA POMBE WALA KILEVI CHOCHOTE NA KWELI SIJAWAHI.
 
Kuber hiyo..😂😂
Kuna bibi mmoja alikua anaitwa bibi’ake Suma kila ikifika jioni ananiagiza duka moja maarufu siwezi kulitaja nitafungua code😂

Sasa mambo ya utoto utoto nikaona anafaidi… siku nikaipasua kidogo nikachota nikamimina kama navyomuona aalivyokua anafanya..

Nilikimbizwa hospitali ya mnazi mmoja 😂😂😂 nilijinyeaaa sitasahau kudadeki😂😂
 
Hahaaaaa hatari sana..
Nilikuwa nashinda kijiweni na masela wanatumia kila aina ya kilevi.
Siku moja nami nikagongea hii kitu...
Kwakweli dakika 5 zilikuwa nyingi, kizunguzungu, jasho mwili mzima yaani sijielewi kabisa.
Nilijikimbiza home nikanywa maziwa fresh nilitapika vya kutosha, nikapiga usingizi wa maana.
Sikurudia tena.
 
2001 hukuwa na umri was kujielewa.Umefurahisha kijiwe tu. Et umesahau simu nyumbani kwa demu wako 🤣🤣 wakati huo simu sio kitu cha kila mtu anayo. Then unasema 500 kuber!!! Unaijua mia 5 ya mwaka 2000?? Kumbuka mtoto wa kishuaa ndio anaenda shule na 50. Hapo ananunua embe la kukata sh 10 au zima sh 30. İnaweza kupata maji ya kifuko sh 5, ubuyu sh 5,muhogo sh 5. Tumenunua sana Kuber kwa hela za shule haikufika jero. Bia yenyewe haikuuzwa jero mwaka 2000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…