Vijana kutoka nchi 8 za Afrika wameongea na wanaanga wa China walioko kwenye Kituo cha Anga ya Juu Tiangong kwa njia ya mtandao.
Wanaanga hao wakiwemo Chen Dong, Liu Yang na Cai Xuzhe wamejibu maswali yaliyoulizwa na vijana hao kama vile wanaweza kuona Jangwa la Sahara na Mlima Kilimanjaro kutoka anga ya juu, jinsi wanaanga wanawake wanavyotimiza ndoto yao, maisha ya angani yanakuwaje, na wanajiburudisha vipi huko angani.
Hii ni moja ya shughuli za kuadhimisha miaka 20 tangu China ianzishe uhusiano wa kibalozi na Umoja wa Afrika.