Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

View attachment 2707633

Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.

Sina maana ya kusema vijana wote wa Arusha ni wahuni na waalifu ama kusema Arusha si salama kabisa, La Hasha! ni kwamba hata katika hao wahuni wachache wanaofanya Arsusha ishuke katika hali ya usalama na maadili, kasi yao ya ukuaji ni mithiri ya kansa ya kidole inavyosambaa mwilini kwahio sio jambo la kufumbia macho kwamba eti kwasababu sio wote basi wapuuziwe, kumbuka hata mayai machache yaliyooza yatazidi kuozesha mengine hatua zisipochukuliwa, kwa wale tuliosoma soma nadhani tunajua kitu kinaitwa compounding.

Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.


matokeo ya kuukuta utamaduni wa kutukuza uhuni kwa vijana wa sasa tangu wakiwa wadogo ndio huchangia zaidi vijana kuendeleza huu utamaduni, Mazingira pia ya jamii inayowazunguka na Mifumo ya malezi kwa baadhi ya wazazi nayo inachangia kukuza vijana wahuni, imeshakuwa ndani ya mfumo wa maisha wa vijana wengi kwamba ili uonekane mjanja basi uwe mhuni ama mhalifu.

mapikipiki haya ya wanakimbiza vibaya mno, ajali kila siku, wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika miguu,.Bodaboda za kutaftia riziki wanalazimisha ziwe pikipiki za michezo, ukienda kwenye magroup yao haya ya kudandia pikipiki kuna "pumzika kwa amani / rip" nyingi sana.

vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo makundi yanaponza sana na kuchangia abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana wamepinda ili kupata uhakiki kutoka wenzao kwamba ni wajanja, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.

Kuna Umakundi makundi wa kihuni huni wanaoishi bila future,

Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye mabifu ama ugomvi baina ya vijana, niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu nje nje,kuna clip nimecheki majuzi Fidovato analalamika vijana wanapigana beto, hata wasanii wa huko Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu, nae Lord Eyes aliwahi kujeruhiwa,

Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.

Suala la maadili nalo limepungua sana na hii imechangia sana hata makanisani na misikitini kuwepo na upungufu mkubwa sana wa vijana,
Kuna msiba vijana wameshiriki mazishi ya mwenzao mara wakataka mchapa mchungaji kisa mchungaji aliwapa maneno ya kweli, sehemu nyingine wamekatisha misa kanisani wakachukua maiti kwenda kuizika wenyewe, kuongea hovyo hata mbele ya camera mpaka hivi sasa imekuwa kama jadi yao hata kama wanaweza kuongea vizuri

Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference
Haya ni majeshi tarajiwa ya kuiondoa CCM madarakani siku zijazo. Dar nako wako. Ni matokeo ya serikali kutokuwa na mpango endelevu wa kuendeleza nchi. Nasikia bandarini kuna pikipiki nyingi zinakuja zina picha ya Samia ili kuhonga vijana uchaguzi ukifika. CCM inajichimbia kaburi na kuna siku nchi haitakalika. Ubaya ni kuwa watu kama kina Samia watakimbilia Uarabuni na kuwaacha wananchi wa kawaida wakitaabika.
 
Sehem yenye exposure mambo ya kusalimiana yashapitwa na wakat...we unataka kusalimiwa ili ikusaidie Nini?nenda huko duniani uone kama Kuna mtu mweny kumind buznss na mtu
Screenshot_20230804-182420.jpg

Nakuona mzee wa exposure unanoa panga arif...!
 
Sasa hivi niko kijiwe cha kahawa hapa karibu na Amana Bank kama unashuka kwa Benson,amekuja dogo kapaki pikipiki ana kiatu kama tofali aisee,kasuruali Kate kamebana chini kama soksi,koti kubwa halafu mchafu mbaya,yaani aisee,siwezi hamishia watoto wangu hapa wakakulia hapa hapana,nina zaidi ya miaka kumi nafanya kazi hapa lakini sipahitaji kifamilia hata kidogo
Wengi wachafu yaani mtu kavaa nguo kibao zimepauka kama zimefuliwa na maji ya chumvi
 
Sijakataa man ndio maana silalamikagi kuhusu mambo za bandari na muungano
Vijana wa Dar wangekuwa kama vijana wa CHUGA sidhani kama Samia angethubutu kuuza Bandari!! Ingawa Kikwete na Kinana waliuza mbuga za wanyama!!
 
nakumanya ile yenyewe we mamsi rudisha kwanza hilo libandari ndo tubonge acha kupiga lomoni nyingi .
Ndugu unadhani kutukana na kuongea kwa lugha ya kipuuzi ndo ujanja? Mimi nimezaliwa Arusha na kukulia mjini kabisa sio huko Kwa morombo, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni au maeneo mengine ya pembeni. Miaka ya 90 mwishoni hadi 2000 mwanzoni swaga za vijana wa Arusha zilikua kuishi kimarekani... hata mavazi yao yalikuwa ya gharama ili kuendana na waamerika. Sio huu upuuzi wa kuvaa matambara na kujiita chalii wa R. Pia kama ni bangi ilikuwa inavutwa tu lakini mambo mengine yanaendelea na huwezi kujua. Enzi zetu watu walikuwa wanavuta bangi lakini lazima uwakute tuition Arusha Sport halafu baada ya tuition tunaenda pale mtoni karibu na kanisa la St Theresa kula mihogo.. hawa vijana wa sasa hivi kazi hawataki na shule hawataki.
 
Back
Top Bottom