Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Haya ni majeshi tarajiwa ya kuiondoa CCM madarakani siku zijazo. Dar nako wako. Ni matokeo ya serikali kutokuwa na mpango endelevu wa kuendeleza nchi. Nasikia bandarini kuna pikipiki nyingi zinakuja zina picha ya Samia ili kuhonga vijana uchaguzi ukifika. CCM inajichimbia kaburi na kuna siku nchi haitakalika. Ubaya ni kuwa watu kama kina Samia watakimbilia Uarabuni na kuwaacha wananchi wa kawaida wakitaabika.
 
Wengi wachafu yaani mtu kavaa nguo kibao zimepauka kama zimefuliwa na maji ya chumvi
 
Sijakataa man ndio maana silalamikagi kuhusu mambo za bandari na muungano
Vijana wa Dar wangekuwa kama vijana wa CHUGA sidhani kama Samia angethubutu kuuza Bandari!! Ingawa Kikwete na Kinana waliuza mbuga za wanyama!!
 
nakumanya ile yenyewe we mamsi rudisha kwanza hilo libandari ndo tubonge acha kupiga lomoni nyingi .
Ndugu unadhani kutukana na kuongea kwa lugha ya kipuuzi ndo ujanja? Mimi nimezaliwa Arusha na kukulia mjini kabisa sio huko Kwa morombo, Moshono, Kisongo, Ngaramtoni au maeneo mengine ya pembeni. Miaka ya 90 mwishoni hadi 2000 mwanzoni swaga za vijana wa Arusha zilikua kuishi kimarekani... hata mavazi yao yalikuwa ya gharama ili kuendana na waamerika. Sio huu upuuzi wa kuvaa matambara na kujiita chalii wa R. Pia kama ni bangi ilikuwa inavutwa tu lakini mambo mengine yanaendelea na huwezi kujua. Enzi zetu watu walikuwa wanavuta bangi lakini lazima uwakute tuition Arusha Sport halafu baada ya tuition tunaenda pale mtoni karibu na kanisa la St Theresa kula mihogo.. hawa vijana wa sasa hivi kazi hawataki na shule hawataki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…