Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Hata kwenye jamii uliyotokea hawakosekani vijana wa hivyo....hatujatofautiana...ni vile tu ushhakuwa na negativity kuhusu ukanda huo
Sio vijana tu hii inaathiri mpaka watoto kizazi na kizazi wanakulia humo mzee. Ukweli mchungu lazima usemwe...!
 
Kuna mwingine tumemzika wiki imepita alinunuliwa boda ..speed zke tulijua hata miezi 3 hamalizi na kweli alikua speed na mwenzake wakagonga basi kwa nyuma wote palepale
 
Niliishi Arusha kuanzia mwaka 2012 mpaka 2014 kwa kweli niliupenda sana huo mkoa kuanzia watu wake, hali ya hewa, vyakula n.k. Ni moja kati ya mikoa ninayotamani kuitembelea tena. Arusha watu wengi ni wastaarabu sana japokuwa wahuni wapo lakini uhuni ni kila sehemu.

Mkoa ambao sipendi kuishi ni Dodoma, Iringa na Njombe na hata Mbeya hii mikoa haijanibariki kabisa.
 
Bangi na Double kick zilishapanda vichwani mwao.
 
boda boda guys are full of comic which turn to perish themselves.Several cases as case study in this year,the government should take measures to rescue their life without that 'll endanger the prosperity of region and country in general!
that with the ongoing spread of gangs and crime will really hurt Arusha in years to come, they may seem little problems as for now but they are compounding at a high rate, the teenagers are badly influenced to glorify these toxic cultures,
 
Hao kelele tu na pikipiki,vichaa wako mbeya bwana,mbeya kuna vichaa na wanajielewa,wamepinda haswaaa hadi wazee
 
Exactly 💯
 
Kwamba unatakasema we familia Bora ??
 
Mkuu hao sio wachaga kwa asilimia kubwa hao ni wameru na wamasai, wachaga wanajua kulea vijana wao na wanaadabu sana, nimeishi kilimanjaro nafahamu hilo. Vijana wengi wa Arusha ni wa hovyo sana kifupi kulea familia Arusha ni ngumu kweli. Kunahitajika operasheni ya kutokomeza hao wahuni la sivyo hata utalii utashuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…