Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Hii iliwahi kunikuta nilipanga kwenye nyumba ya mzee mmoja hivi basi nilishangaa kuna vijana fulani ni kama ndugu zake yule mzee na wengine nadhani walikuwa wasaidizi wa kazi za nyumbani kwa mzee,hao vijana umri wao ni kama miaka 16 hivi.
Imagine tulikuwa tunaishi kwenye nyumba moja na tunashea sebule lakini hawajawahi kunisalimia hata siku moja tulikuwa tunapitana tu kwa muda wa miezi 6 niliyokaa pale.
Hii kitu ilinishangaza sana.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo yupi mjanjanja zaidi ya mwenzie!!?? Mchaga au Mchugaa!!??
Inategemea ni ujanja kwenye nyanja ipi.
Kwa jinsi nilivyowasoma mimi tofauti kati ya mchaga na Mchuga/Muarusha ni kwamba wa wachaga anajali muda na kusaka noti wakati Waarusha wanapenda kukaa maskani na kusimuliana stori za matajiri kama ni kazi wanayoiamini ni kwenda mererani kusaka madini au kupeleka watalii mbugani.
Utasikia wakisimuliana "Yule jamaa achana naye chalii yangu ni ana hela chafu,usiniambie arifu eeh si alikuwa mererani huko akaokota jiwe"
Pia wakipata hela wanaiga life la matajiri wenyewe wanaita mabilionea yaani kwa mfano akibahatisha laki 5 ataenda baa alipie friji lote la baa na kuamuru baa ifungwe bia zote zimenunuliwa na Ze don[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 

Acha tu kiongozi Wana ustaarabu wa hovyo sana...!
 
Muache kuja arusha banaa [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] kama arush yetu inawaboa hizi swaga ni sehemu ya maisha kwetu
 
nina asili ya moshi ila nimezaliwa na kukulia arusha kipindi chote cha utoto, mpaka kuingia ujanani, anayesema huyu ni kweli kabisa, ila wanaosema arusha sio sehemu yakuwa na familia wanakosea, muhimu omba tu upate mtoto asiyefata mkumbo, mimi nimekaa na machalii yangu wa kitaa wamepinda mbaya wanakula kila kitu at our age lakini mimi sikuwahi kushawisha kuwafata katika mambo yao ili kupata approval, sio shuleni boarding au wapi, ni mimi tu na misimamo yangu na nikatoboa mpaka mambele kusoma nk ila nimepitia na nimeishi mitaa iliyopinda mno, sinoni daraja mbili, kijenge juu, ungaleloo kote huko tuliwahi familia yetu iliwahi kuishi kabla wazee kutoboa nakuhamia maeneo ya utulivu na ustaarabu kidogo ...ila mpaka sasa sijawahi kuvuta bangi, kula kuberi, kuvuta fegi, kunywa kiroba nk
 

[emoji15][emoji15][emoji15][emoji134][emoji134][emoji134][emoji2088][emoji2088][emoji2088]
Kumbe ni wa chugga wewe??
 
Arusha miaka yote iko hivyo...
Uhalifu unaabudiwa

Kuna familia maarufu za ujambazi...

Arusha ... wanahitaji zaidi exposure ya dunia ....
Wale kupakana na kenya ndio tatizo hasa kuwa karibu na nairobi
 
Fata mambo yako jomba temana na raia waishi life lao dingilii!

Mbona huko kweni kumejaa wachawi na hatubongii!

Unakuja hapa eti Arusha Arusha kama vipi tuachieni Arusha yetu tuamie kenya

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 

Inawezekana, kipindi cha Magu Arusha ilikuwa tofauti sana. Machokoraa pia walipotea.

Lakini sasa Arusha kuna mitaa roho mkononi, polisi wanakila sababu ya kuwajibika na uhuni unaoendelea kufanyika.

Maadili yanajengwa ama kwa kuelimishwa laa kwa shuruti.
 
Kuna mkoa gani ambao hauna wahuni na hayo mambo hayapo? Embu nitaajie ndio nitajua arusha kweli ni tatizo linalohitaji tiba.
 
Arusha wanajikutaga wapo jimbo la California huko Compton ndani ndani ...mitaa ya kina The Game ilipozaliwa NWA.

So nao wanafanya gang banging sema hawana bunduki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…