Vijana wa Arusha kuuona uhuni na usela ni ujanja kunazidi kulitafuna jiji, usalama umepungua, maadili yameshuka, serikali haina msaada

Uko sahihi sana mleta mada. Arusha ujinga ni mwingi na unatukizwa. Malezi mabovu ndio chanzo natokea kilimanjaro lakini majirani zetu kunasehemu walifeli japo vichwa vipo kuna madogo ni wapambanaji alafu wako smart sana.

Bhange na pombe kali sikatazi mtu kutumia ila makundi yanaponza sana
 
Ndio maana hayati Nyerere alidai uhuru kwa kuanza kuwahusisha watu wa pwani ,kati ,kusini na nyanda za juu....

Hapa kuna siri kubwa mno....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Watu wa pwani ndio waliomuhusisha Nyerere na Sio Nyerere ndie, baada ya Uhuru aliipotosha historia.
Yeye alikuta tayari harakati zimeanza wakampa uongozi wa chama kwa sababu tu ya usomi wake.
Uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya makubaliano ya wazee wa pwani na shetani mapangoni bagamoyo ikiwemo masharti Kama uwepo wa umasikini,mbio za mwenge,nk
 
Uko sahihi sana mleta mada. Arusha ujinga ni mwingi na unatukizwa. Malezi mabovu ndio chanzo natokea kilimanjaro lakini majirani zetu kunasehemu walifeli japo vichwa vipo kuna madogo ni wapambanaji alafu wako smart sana.

Bhange na pombe kali sikatazi mtu kutumia ila makundi yanaponza sana
Kilimanjaro dini ndio imewasaidia kuwashape mlivyo.Hadi miaka ya 2000 mabinti wengin walimaliza sekondari wakiwa bikira kabisa.
Wameharibika ni baada ya ujiio wa mmomonyoko wa maadili wa kidunia wa kizazi hiki
 
Watu wa pwani ndio waliomuhusisha Nyerere na Sio Nyerere ndie, baada ya Uhuru aliipotosha historia.
Yeye alikuta tayari harakati zimeanza wakampa uongozi wa chama kwa sababu tu ya usomi wake.
Uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya makubaliano ya wazee wa pwani na shetani mapangoni bagamoyo ikiwemo masharti Kama uwepo wa umasikini,mbio za mwenge,nk
Inasikitisha sana
 
View attachment 2707633

Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.

Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wnyaturu.

jamii za mikoa ya karibu waliohamia Arusha kwa muda mrefu (sio wakuja). hapa wapo Wameru, Waarusha, Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.

matokeo ya kuukuta utamaduni wa kutukuza uhuni tangu wakiwa wadogo, imeshakuwa ndani ya mfumo wa maisha wa vijana wengi kwamba ili uonekane mjanja basi uwe mhuni wa kunywa pombe kali, kuvuta bangi ama uwe mhalifu.

mapikipiki haya ya wanakimbiza vibaya mno, ajali kila siku, wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika miguu,.Bodaboda za kutaftia riziki wanalazimisha ziwe pikipiki za michezo, ukienda kwenye magroup yao haya ya kudandia pikipiki kuna "pumzika kwa amani / rip" nyingi sana.

vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo ni pale wanatumia vilevi kupita kiasi na ku abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana mzoefu ili kupata sifa za kuonekana ni moja wao, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.

Makundi ya vijana wengi ni magenge ya vijana wanaoishi bila future, wanafanya vingi bila kujali madhara wala kesho.

Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye mabifu ama ugomvi baina ya vijana, niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu nje nje,kuna clip nimecheki majuzi Fidovato analalamika vijana wanapigana beto, hata wasanii wa huko Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu, nae Lord Eyes aliwahi kujeruhiwa,

Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.

Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference
Wewe unaijua Arusha na watu wake. Tunakupa maua yako. Kwenye mpango mkakati wa kuiokoa Arusha unatakiwa uwe team member au team leader kabisa.
 
Nimekulia Arusha, naishi dar, nina miaka 53, hayo ya Arusha nayaona kwenye simu, sijawahi yaona in real life, ni % ndogo sana.
 
Back
Top Bottom