Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Mbona machalii wa kisongo wako poa jombaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha Umbea kijana wa Daslam mshindia kiepeArusha vijana wa kiume ndio wanaoongoza kwa kuliwa na wanaume kwa mikoa ya Bara, pia kuoa vibibi vizee.
Kama upo mbali na Arusha, Uhuni wao unakuwasha nini?Masela “nya” , ila uzuri wakiingia Daslam ushenzi wao wanauachaga kwenye mabasi, shwaaain kabisa. [emoji706][emoji706]
Hakuna kitu kama hichoMbon zipo tu nilikua naangalia clip moja Fido analalamika machalii wanapigana sana beto
Una mifano hai?Unataka kusema kwa starehe zilivyo arusha...vijana hawatafuniki kabisaaaa ?!! [emoji1787][emoji1787]
Unataka kusema kusema WAZUNGU wenye tabia za "LGBT" wanaishia tu Dar na kwengineko ?!!! [emoji1787]
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ujanja au Uhuni wao unakuathiri vipi wewe uliye mbali?Wale watoto wanajiona wajanja sana
Mkuu umenijibu jana umeona nimekukalia kimya leo umerudi tena kuna unachokitafuta? By the nipo njiro arusha na leo nina muda na mood ya kutosha.Kama upo mbali na Arusha, Uhuni wao unakuwasha nini?
Si uwaache waishi kivyao?
Hilo nalo nenoInashangaza Mtu yupo mbali na Arusha na yupo mbali na Vijana wa Arusha kwa some kilometers away lakini bado anaumizwa na lifestyle ya watu
Arusha isipothibitiwa itakuwa kama Durban Africa KusiniView attachment 2707633
Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.
Sina maana ya kusema vijana wote wa Arusha ni wahuni na waalifu ama kusema Arusha si salama kabisa, La Hasha! ni kwamba uhuni ni kama umefumbiwa macho usambae mithiri ya kansa ya kidole inavyosambaa mwilini kwahio sio jambo la kufumbia macho kwamba eti kwasababu sio wote basi wapuuziwe, kumbuka hata mayai machache yaliyooza yatazidi kuozesha mengine hatua zisipochukuliwa, kwa wale tuliosoma soma nadhani tunajua kitu kinaitwa compounding.
Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.
Huu utamaduni wa kutukuza uhuni sijui ulifika vipi huu mkoa lakini unazidi kuleta athari kubwa, ulianza kidogo ila unazidi kukuzwa na kufanywa na vijana wengi wa sasa walioukuta tangu wakiwa wadogo, Mazingira ya jamii inayowazunguka na Mifumo ya malezi imekuwa mstari wa mbele kuwa kichocheo.
Kijana akiwa mhuni ama muhalifu ni jambo analoweza kujisifia na kupewa heshima, akienda jela ni kama cheo kabisa kisicho na shaka kwamba aliwahi kupiga tukio.
mapikipiki haya yanakimbizwa vibaya mno ili tu kupata sifa, vijana wanapoteza maisha kwa sifa za muda mfupi, tena sikuhizi kumezuka makundi ya kuendesha kwa kuinua tairi, Mbaya zaidi hawavai uniform za kujilinda ama kutumia pikipiki maalum za michezo, wanatumia bodaboda hizi za kichina za kubebea abiria na hapo hana jaketi gumu, hana kiatu kigumu kirefu, hana begi la sponji kulinda mgongo, hajavaa gloves za mikono, hana guard za viwiko na makoti, hana hata helmet kavaa mzula wa baridi ila anadiriki kuendesha kwa kasi ama / na kunyanyua tairi la pikipiki isiyo ya michezo, ajali hizi za kujitakia zipo nyingi vijana wanazikwa kama kumbikumbi, wengine wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika....
vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo makundi yanaponza sana na kuchangia abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana wamepinda ili kupata uhakiki kutoka wenzao kwamba ni wajanja, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.
Kuna Umakundi makundi wa kihuni huni wanaoishi bila future,
Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye ugomvi , niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu inamwagika, hata wasanii wa huko kina Lord Eyes na Fido Vato wamewahi kupigwa visu,Marehemu Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu.
Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.
Suala la maadili nalo limepungua sana na hii imechangia sana hata makanisani na misikitini kuwepo na upungufu mkubwa sana wa vijana,
Kuna msiba vijana wameshiriki mazishi ya mwenzao mara wakataka mchapa mchungaji kisa mchungaji aliwapa maneno ya kweli wakachukua maiti kwenda kuizika wenyewe, kuongea hovyo hata mbele ya camera mpaka hivi sasa imekuwa kama jadi yao, mavazi wanayoona yanayomwakilisha mwana arusha original ni kuvaa mashati marefu mpaka magotini pamoja na miviatu mikubwa kuliko size za miguu.
Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference
Ikiwa ni nchi moja basi tambua kuna mwingiliano sana mfano kimahusiano,kibiashara kirafiki na hata kidini...lakini inapotokea hata mwenyeji anakosa amani kwa mgeni wake tokana na tabia za kishenzi za eneo lake kwa mgeni unategemea atafsiri nini ?Why So obsessed na visivyowahusu 🤭🙃
Arusha kwa sasa kuna ufirauni kuliko hata pwani. wazungu wamewaharibu mno, na mabange.dar vijana wanashindana na wadada kwa urembo, wengine wanakulana
hili mbona hatulizungumzii??
Hahaha, hunifahamu....karibuMkuu umenijibu jana umeona nimekukalia kimya leo umerudi tena kuna unachokitafuta? By the nipo njiro arusha na leo nina muda na mood ya kutosha.
Au unataka mkono?Mkuu umenijibu jana umeona nimekukalia kimya leo umerudi tena kuna unachokitafuta? By the nipo njiro arusha na leo nina muda na mood ya kutosha.
Lete mfano kama unaoArusha kwa sasa kuna ufirauni kuliko hata pwani. wazungu wamewaharibu mno, na mabange.
Watu wame overrate humu. Usiamini kila unachokisikiaIkiwa ni nchi moja basi tambua kuna mwingiliano sana mfano kimahusiano,kibiashara kirafiki na hata kidini...lakini inapotokea hata mwenyeji anakosa amani kwa mgeni wake tokana na tabia za kishenzi za eneo lake kwa mgeni unategemea atafsiri nini ?
Yaani kila kitu unachofanya kina warning unapewa..kuanzia njia/ barabara,mitaa,urafiki,gereji unapopeleka chombo cha moto kwa matengenezo,Bar hadi lodge...yaan mpaka unajiuliza hawa vijana ndio wanaoleta shida hii ya watu kuna wasi wasi all time...!!!
Kuwa serious mkuu. Hali ya Arusha siyo kabisa. Hata hayo matendo unayosema yanafanyika kule Dar, Arusha napo yapo na zaidi imekua kama sehemu ya life style kwao.dar vijana wanashindana na wadada kwa urembo, wengine wanakulana
hili mbona hatulizungumzii??