Vijana wa Dar es Salaam mmekuwaje? Hii ni aibu kwa taifa

Vijana wa Dar es Salaam mmekuwaje? Hii ni aibu kwa taifa

Kwa muda wa takribani wiki mbili tangia niingie Dar es salaam nimejikuta na duwaa kwa kuwashangaa vijana na wanaume wanaovaa vipensi vifupi vinavyoonyesha mapaja.
Je?
Msingi wa jambo hili ni nini maana kimaadili halijakaa sawa.
Hivi ni kweli vijana hawa hawaishi na watu wazima ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa maadili.
Hii ni aibu kwa taifa hasa ukizingatia jiji hili linapokea watu wa aina mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.
Vijana tuache ulimbukeni kwani si kila jambo linalozuka ulimwenguni ni la kuiga mengine yanatushushia heshima hasa katika jamii inayotuzunguka .
Sisi watu wa vijijini tumekua tukiambia dar kuna wajanja kama huu ndo ujanja wenyewe nibaki kuwa mshamba milele na wala sitadhurika na ushamba na wala sio huu ujinya.
Sisi ndo tunatakiwa tuwe mfano bora wa kuigwa kwa watoto wanaokuwa kwa sasa.
Haya si maadili wala mila zetu.
NB:najua wahusika mtakuja kunishambulia kwa fujo ila ukweli ndio huo
Mjini mambo mengi muda mchache. Sasa hivi vijana wa kiume wanasuka nywele au kupaka rangi, kutinda nyusi, kutoga masikio, kujikoboa, kupaka kucha rangi, kuvaa vipedo, chips kwa wingi,mahindi ya kuchoma kwa ndimu na pilipili n.k.

Siku hizi wanashindana kutikisa miwowo na dada zao.

Kibaya zaidi wengine wana- practice ushoga, kuoa au kuolewa na vikongwe n.k.

Mitaani ugomvi hutokea kati ya mabinti zetu na kaka zao wakigombea mabwana.

Hizi tamaduni za kimagharibi zimeharibu sana vijana wetu.

Baada ya miaka michache tutakuwa na nguvu kazi chache sana ya vijana kwa tabia hizi.

Sheria ziwekwe,atakayezikiuka ashughulikiwe, mfano nchi za Kiarabu hakuna huo ujinga ujinga. Huenda tukatibu hilo tatizo kwa vijana wetu.
 
hao viongozi wakulalamikiwa watoto wao ndo wahusika wakuu unafikiri wanaweza fanya kitu ambacho kitawaumiza baadaye.
 
Hapa Tanzania hatuna watu walio makini Kama hapa Daslama. Acha wavae vipensi Joto Ni Kali Sana sijui mnasemaje hapo.
 
Kama hawa??
Kings African Rifles Parade Tanganyika 1956.jpeg
 
Wewe Karumanzila, maliza kuuza hayo matikiti maji ili urudi mapema kwenu Kisiju. Mambo ya watu wa Dar waachie wenyewe!
Mengi tu tunawaachia wenyewe lakini sio swala la ushoga tunakataa na tunalikemea vijana wa dar kwa hii miaka 10 mnazidi kupoteza Maadili na ushaid upo
 
Ishi maisha yako mkuu, mwanaume halei... akili za mtoto mara nyingi ni za mama so anza kwanza kuwaelimisha kwanza wanawake wa siku hizi waache kuvaa nguo zisizo na maadili.
 
Sisi tunaotoka vijijini tunapata shida sana kuwaangalia vijana wa daslam, unajiuliza maswali mpaka unakosa majibu.......hapa Tarime unakula fimbo kabisa
 
Back
Top Bottom