Vijana wa Dar es Salaam mmekuwaje? Hii ni aibu kwa taifa

Vijana wa Dar es Salaam mmekuwaje? Hii ni aibu kwa taifa

Dar si ndo kama new York au ulikuwa hujui ww
 
Kina bdozen wa Efm si wanaliwa wale sasa watu wanawaiga kwakua ndo upande wa dunia waliochaguliwa kuuona
 
Kwa muda wa takribani wiki mbili tangia niingie Dar es salaam nimejikuta na duwaa kwa kuwashangaa vijana na wanaume wanaovaa vipensi vifupi vinavyoonyesha mapaja.
Je?
Msingi wa jambo hili ni nini maana kimaadili halijakaa sawa.
Hivi ni kweli vijana hawa hawaishi na watu wazima ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa maadili.
Hii ni aibu kwa taifa hasa ukizingatia jiji hili linapokea watu wa aina mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.
Vijana tuache ulimbukeni kwani si kila jambo linalozuka ulimwenguni ni la kuiga mengine yanatushushia heshima hasa katika jamii inayotuzunguka .
Sisi watu wa vijijini tumekua tukiambia dar kuna wajanja kama huu ndo ujanja wenyewe nibaki kuwa mshamba milele na wala sitadhurika na ushamba na wala sio huu ujinya.
Sisi ndo tunatakiwa tuwe mfano bora wa kuigwa kwa watoto wanaokuwa kwa sasa.
Haya si maadili wala mila zetu.
NB:najua wahusika mtakuja kunishambulia kwa fujo ila ukweli ndio huo
Hao vijana wanajiuza.
 
Mtoa mada kumbuka kuna kitu kinaitwa privacy , na kuna private life pua ambayo naamini hata wewe usingependa kuingiliwa
Picha nyingi zilizotumwa humu ni kwamba watu wapo sehemu zao private , hawapo kanisani msikitini au sehemu zozote sensitive kusema kwamba wataharibu maadili
Mtu yupo home kapumzika unataka avae casual jeans na kadet ili aonekane mwanaume?
 
😂 kuna mmoja tulikaa siti moja wiki iliyopita DAR-MBEYA niseme jamani ile ni boxer😄 sasa alivo bonge niko sit ya dirishani kajitanua huyooo na umbaumbau wangu kidogo anitolee dirishani sio kwa kunibana,,, akili ikajiuliza inakuwaje ndani ya basi kunaAC n tumetoka alfajiri tuendako ni mji wa baridi hii bukta vip,,, 😂😂 nikaukumbuka ule uzi wa wanaume wa GYM na matukio yao nikajisemea hii safari huyu bwana hajainjoi alijua siti mwenza angekuwa mwanaume mwenzake huenda angepata danga.
 
Kumbuka Dar kuna joto sana.Mbona wacheza mpira wa soka wanavaa kaptura hilo huoni.Ushamba wako wa bara usiwaambukize watu wa dar.
Jiulize wewe ni kabila gani halafu ulianza kuvaa suruali lini au kwa kifupi tu chukulia miaka 200 babu zako walikuwa wanavaa nini.Hata kuvaa suruali ni utamaduni tumeiga watu wa nje
 
Unawatamani hayo mapaja yao??
Kwani wachezaji wanavaaje wakiwa uwanjani??

Labda kwa wanawake ila kwa wanaume hivyo vibukta havina athari yoyote ukizingatia na hali ya hewa ya huko.

Vipaja vyembamba, vimekomaa kichizi unaonaje ajabu sasa.

Mwanaume cha kuficha ni mkuyenge na nyuma hayo mengine hata yakae wazi haina shida.
 
vaa suruali mkuu..acha kuvaa vipedo ya kaptula..unajidhalilisha sana
Sivai vikaptula, ila hata nikiamua kuvaa hakuna wa kunizuia. Maana sivunji sheria, wala siendi kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania!
 
Wanaotetea huu upuuzi wa wanaume kuvaa vibukta vifupi ni wao wao
Ndio ukichunguza sana mashoga wengi wanakuwa ni wao wanaotetea huu ujinga
Kuna pensi za kuvaa mtoto waokiume imevuka kwenye magoti pia ina nafasi nasio kafupi na chakubana badilikeni acheni ujinga huo sio ujanja kama mnavyojua
 
Hawa vijana unaosema wanavaa hizi nguo siyo wengi ama sivyo tungewaona.
Na hiyo nguo unayolalamika haonekani kama Ina madhara yoyote.
Hapo usichanganye vitu viwili: yule aliyevaa buktha na yule anayelegeza mshipi
Haya mambo yalijadiliwa zamani,na vijana wa CCM wakawa wanawashambulua hawa watu.
Halafu wazee wa CCM wakaamua kwamba vijana hawa siyo wengi. Tusijiletee uadui na wananchi bila sababu.
Jana,nilikuwa nafikiria,kwa mfano, pornography,ipo katika internet. Kwa nini Serikali haijaipiga marufuku.? Obviously kwa sababu wananchi wenyewe wanaonekana ni sensible na wanaweza kuamua jambo la kufanya
 
Back
Top Bottom