Vijana wa Dar, wakiwaona wazee kwenye daladala, wanajifanya wamelala

Vijana wa Dar, wakiwaona wazee kwenye daladala, wanajifanya wamelala

Wazee wanakera, anaona kabisa basi limejaa..alafu anapanda akijua kuna mtu atampisha...ukinikuta mimi utasimama sana mzee
Kumbuka kuwa, hata wewe hautabaki kijana miaka yote.
Kwa changamoto za usafiri wa daladala za hapa Bongo huo ubavu wa mzee kusukumana na vijana kugombea kupata siti anautoa wapi?
 
Vijana wa Dar, wakiwaona wazee kwenye daladala, wanajifanya wamelala, lakini wakiona kijana mwingine wanajua kupiga haraka speed za 'Formula 1'!"
🤗
Mimi huwa nikienda kwenye mikusanyiko ya watu mfano msibani, huwa najiwahi kukaa mfano kwenye msingi au tofali.

Kamwe sikalii kiti mana najua ntaona aibu kumpisha mzee. Nikikaa kwenye msingi hapo sina kosa, akija mzee nauchuna tu apambanie viti kwanza vilivyokaliwa na vijana.
 
Wanatafuta huruma. Asilimia kubwa huwa napanda gari stand. Unakuta gari limejaa ndo anaingia mzee,mjamzito au mama mwenye mtoto akitegemea watu watampisha,wakati huo huo unaona limekuja gari tupu yaan hata kujikurupusha ashuke apande hilo wala hana hilo wazo anakuja kuegamia ulipo
😩shida huwa n nini kwa upande wako
 
Back
Top Bottom