Tatizo la CCM waliwatupa wazee waasisi wazee waliokishauri chama, wakakumbatia vijana. Sasa wanalazimisha vijana wawe wazee washauri wa chama. Vijana wanagombea upigaji.
Mliona bunge la chama kimoja, Wabunge dhidi ya Mawaziri walishambuliana haswa, ile haikuwa drama bali vita. Pale unapata picha ccm imebaki mabua.
Yani wana raruana kisawa sawa hakuna wa kuwa kanya, Majaliwa alikuwa bungeni siku hizi haogopwi tena, aliogopwa enzi za Magufuli lakini sasa unaona wanafahamu hana nguvu tena.
Kinana, anakifahamu chama vilivyo, kwa nafasi yake kaamua kuangalia tu, na kusubiria kuondoka bila lawama, na soon ataagwa.
Hao mnao waita vijana wa Magufili nao Chali, wakiitisha mkutano nao utasikia wanaomba suport ya Mama awepo, bila hivyo mahudhurio ya wananchi ni zero.
Mama anjipigania mwenyewe, hataki makundi lakini pia hawezi kusuluhisha maugomvi peke yake. Msoga naye anapwaya, hawezi kumsaidia zaidi ya kumshauri awapuuze tu aendelee kuchapa kazi.
Chama hakina mwenyewe, watakikabidhi kwa Polisi, na wakishindwa watapewa JWTZ.