Vijana wa Kenya (Gen Z) sasa mnataka nini?

Vijana wa Kenya (Gen Z) sasa mnataka nini?

exactly! demand yao amesalimu amri, sasa why gen z turn violent?
Siku nyingine kama anakubali kitu akubali, kama anakataa akatae jumla.. Juzi ametoka akawafokea akaona hawajaogopa, ndio akaja kujifanya amewasikiliza.. kiongozi mwenye ndimi mbili hawezi aminika.

Toka mwanzo hii Bill walitaka kuipitisha kidictator na rushwa... kuna wabunge wamehongwa 2M ya Kenya, some of them wamevunjiwa makazi yao na waandamanaji, Wale vijana hawatanii.... wakitaka wawaue kila nyumba itakuwa na msiba.

Viongozi watumie busara kukiri kuwa walikosea, then warudishe muswada bungeni ukajadiliwe upya.
 
Wanataka serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima, kuanzia safari za nje, bajeti ya hela za (confidential), kawaida na ujinga na uozo wote.

Wanataka rais akubali na atoe pole kwa wafiwa 20 plus waliouwawa.

Wanataka kodi zao na matumizi yake yaelezewe..

Ubabe na ujinga wa kunyamazisha vyombo vya habari ukome..
copy ya haya maandishi ibaki kwa chief hangaya
 
Wakenya ni wapuuzi, vitu ambavyo vinazungumzika kwa njia ya demokrasia wao wanaona sifa kufanya vurugu,

Wamechagua ugali maharage na pilipili tena kwenye vita.

Kingine jeshi la kenya ni dhaifu sana tena dhaifu mno.
 
Siku nyingine kama anakubali kitu akubali, kama anakataa akatae jumla.. Juzi ametoka akawafokea akaona hawajaogopa, ndio akaja kujifanya amewasikiliza.. kiongozi mwenye ndimi mbili hawezi aminika.

Toka mwanzo hii Bill walitaka kuipitisha kidictator na rushwa... kuna wabunge wamehongwa 2M ya Kenya, some of them wamevunjiwa makazi yao na waandamanaji, Wale vijana hawatanii.... wakitaka wawaue kila nyumba itakuwa na msiba.

Viongozi watumie busara kukiri kuwa walikosea, then warudishe muswada bungeni ukajadiliwe upya.
Nakubaliana na wewe kabisa. Vijana walikuwa sahihi kupinga hiyo kitu ha fedha. Si amesha withdraw bill na hakuisaini? sasa kuvamia bunge kunatoka wapi? wasiwasi wangu ni kuwa kusije kuwa na elements za hooliganism!
 
Wanavuta bangi wanadhani watu wote wana akili za kushinda mitandaoni na kuandika ujinga na wivu, wanaweza wakawa ni wengi lakini bado nchi hizi za afrika mashariki hazijafikia wakati wa kuongozwa na mihemko ya mitandaoni.

Hivi sasa watapigwa kweli kweli na hao wanajeshi , mwanzoni walionekana wana hoja na wanajeshi wakawa wakiwahurumia kwamba wanayo mantiki katika hicho wanachokifanya, lakini wanapoenda watapokea mkong'oto wa uhakika kutoka kwa hao hao waliowaachia wakafanya walichofanya.
Wewe Baki na ujinga wako. Unajifanya una hasira na Wakenya wakati hata bajeti ya nchi yako hujui imepitishwa lini?.
 
Akili za kitoto taabu sana hawawezi kuona kuwa Somalia iliharibiwa kwa akili za namna hii hii za hawa madogo wa Gen Z, watafika mahali kila mtaa utataka kuwa na serikali yake na uporaji unakuwa ndio sheria ya kila siku mtaani.
Somalia iliharibiwa na Viongozi sio wananchi. Kasome historia. Na Kenya inataka kuharibiwa na Ruto.
 
Financial Bill ni nini jamani , inahusu nini na lengo lake nini ? 🤣🤣 Ngoja niulize maana kweli naona wanaandamana na hilo neno ndo Rejista inayotumika sana ! Ila sielewi

Kuuliza si ujinga ! Nisanueni
Sheria ya Bajeti. Yetu imepitishwa Jana na nadhani wengi hawajui Kama Jana tumepitisha finance bill ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom