Vijana wa Kenya (Gen Z) sasa mnataka nini?

Vijana wa Kenya (Gen Z) sasa mnataka nini?

Wanavuta bangi wanadhani watu wote wana akili za kushinda mitandaoni na kuandika ujinga na wivu, wanaweza wakawa ni wengi lakini bado nchi hizi za afrika mashariki hazijafikia wakati wa kuongozwa na mihemko ya mitandaoni.

Hivi sasa watapigwa kweli kweli na hao wanajeshi , mwanzoni walionekana wana hoja na wanajeshi wakawa wakiwahurumia kwamba wanayo mantiki katika hicho wanachokifanya, lakini wanapoenda watapokea mkong'oto wa uhakika kutoka kwa hao hao waliowaachia wakafanya walichofanya.
Mitandaoni wakati watu wapo barabarani? Wakenya sio waoga kama waTanzania hata bungeni zilikua zinapigwa risasi kabisa za AK 47 wakafa 20, ila watu zaidi ya elfu 5 wakavunja geti.

Huwezi kuua waandamanaji laki 5 zaidi utaua mamia na waliobaki watakuvamia. Hakunaga bunduki inayoshinda umma usio na cha kupoteza.
 
Hata aje nani bila a complete overhaul of the current status quo vitu havitabadilika na huku hayo yatatokea punde...

Nguvu kazi katika karne ya sasa haiitajiki tena hivyo ajira ni tatizo na kama ajira ni tatizo katika nchi ya kipebari ambapo means of production zinahodhiwa na wachache wengi hakuna wanachopata (sababu wangepata ujira through ajira) leo hii wanachopata ni wivu tu wa kuona what they can not have.....
Watu wanaongelea bajeti wewe unaongelea wivu. Wivu ni personal bajeti ni national issue.
 
Wanavuta bangi wanadhani watu wote wana akili za kushinda mitandaoni na kuandika ujinga na wivu, wanaweza wakawa ni wengi lakini bado nchi hizi za afrika mashariki hazijafikia wakati wa kuongozwa na mihemko ya mitandaoni.

Hivi sasa watapigwa kweli kweli na hao wanajeshi , mwanzoni walionekana wana hoja na wanajeshi wakawa wakiwahurumia kwamba wanayo mantiki katika hicho wanachokifanya, lakini wanapoenda watapokea mkong'oto wa uhakika kutoka kwa hao hao waliowaachia wakafanya walichofanya.
Mahakama ya juu ya kenya imebatilisha order ya askari jeshi kuwa deployed mtaani
 
Wajaluo wanamtaka Raila full stop

Ukabila Kenya shida
Wewe mjinga kweli. Gen Z hawakuwa na kiongozi Wala kabila ndio maana maana Eldoret ngome ya Ruto maandamano yalikuwa makubwa Sana mpaka kushusha mkokoteni wa UDA ulikuwa katikati ya mji. Pia Nyeri ngome ya Gachagua maandamano yalikuwepo. Usisahau maandamano ya Kiambu eneo la Githurai 45 ambako Wakikuyu wameshambuliwa na polisi. Kwa mara ya kwanza Wakenya wameweka ukabila pembeni wakawa na sauti moja.
 
Lakini kwa mwanasheria as long as Rais hajai sign, then all is Ok! Hakuna kitu hapo, the statu quo remains !

Step by step, amekataa kusain, then with time itafutwa as they demand. sasa kula wali bungeni inaashiria nini?
Mwenye mamlaka ya kuifuta ni bunge sio Rais. So bunge lisipokaa kufuta huo muswada kwa siku 14 inakuwa sheria moja kwa moja. Ni ujanja Ruto anataka kutumia ndio maana wananchi hawamwamini.
 
Madai mengine hayo sasa.

Sidhani kama rais anaweza kuwa mpuuzi kiasi hicho cha kudanganya ili after 21 days iwe operational!
Humjui Ruto, ni mzuri kwenye manipulation na utapeli. Juzi kawatukana waandamanaji, ila Jana kawaita watoto wetu. Leo jeshi limeingia mtaani. Ruto alifaa kwenye ugavana na Uwaziri sio kuwa Rais wa Nchi.
 
Katika siasa za Kenya kuna mambo mengi nyuma ya pazia! Kwanza nani anaratibu kikundi hiki cha GEN Z? Tunajuaje kama ni wanasiasa wenye nia ovu na Ruto? Ok sawa Katiba inaruhusu maandamano Je Katiba inaruhusu uharibifu wa mali za raia na serikali? Tuhoji km rational people!
Uharinifu wa Mali ni moja ya matokeo wakati wa maandamano. Ni kama kucheza mpira waweza kuvunjwa miguu, ila lengo halikuwa kuvunjwa miguu Bali kucheza mpira.
 
There you are! ! Hapo ndipo GEN Z wamevuruga. Walikuwa katika msitari ulionyooka, lkn baada ya kuanza uharibifu, ndiyo nikapose thread hii! Wanataka nini? Rutto aondoke? aje nani?
Kwani wananchi wakitaka aondoke Kuna shida?. Wao si ndio wamechagua. Usilete mambo ya CCM Kenya, serikali ni ya wananchi sio kitu kimeshuka kutoka mawinguni.
 
Huko wanakoelekea sasa wanaharibu, rais kashawasikiliza madai yao na kawaambia watakaa chini kwa pamoja waseme wanataka wafanyaje kuhusu Kenya, lakini wao hawataki.!

Wataiharibu nchi yao ishindwe kukalika kwa mihemko yao.
 
Back
Top Bottom