Vijana wa Kenya (Gen Z) sasa mnataka nini?

exactly! demand yao amesalimu amri, sasa why gen z turn violent?
Siku nyingine kama anakubali kitu akubali, kama anakataa akatae jumla.. Juzi ametoka akawafokea akaona hawajaogopa, ndio akaja kujifanya amewasikiliza.. kiongozi mwenye ndimi mbili hawezi aminika.

Toka mwanzo hii Bill walitaka kuipitisha kidictator na rushwa... kuna wabunge wamehongwa 2M ya Kenya, some of them wamevunjiwa makazi yao na waandamanaji, Wale vijana hawatanii.... wakitaka wawaue kila nyumba itakuwa na msiba.

Viongozi watumie busara kukiri kuwa walikosea, then warudishe muswada bungeni ukajadiliwe upya.
 
copy ya haya maandishi ibaki kwa chief hangaya
 
Wakenya ni wapuuzi, vitu ambavyo vinazungumzika kwa njia ya demokrasia wao wanaona sifa kufanya vurugu,

Wamechagua ugali maharage na pilipili tena kwenye vita.

Kingine jeshi la kenya ni dhaifu sana tena dhaifu mno.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Vijana walikuwa sahihi kupinga hiyo kitu ha fedha. Si amesha withdraw bill na hakuisaini? sasa kuvamia bunge kunatoka wapi? wasiwasi wangu ni kuwa kusije kuwa na elements za hooliganism!
 
Wewe Baki na ujinga wako. Unajifanya una hasira na Wakenya wakati hata bajeti ya nchi yako hujui imepitishwa lini?.
 
Akili za kitoto taabu sana hawawezi kuona kuwa Somalia iliharibiwa kwa akili za namna hii hii za hawa madogo wa Gen Z, watafika mahali kila mtaa utataka kuwa na serikali yake na uporaji unakuwa ndio sheria ya kila siku mtaani.
Somalia iliharibiwa na Viongozi sio wananchi. Kasome historia. Na Kenya inataka kuharibiwa na Ruto.
 
Financial Bill ni nini jamani , inahusu nini na lengo lake nini ? 🤣🤣 Ngoja niulize maana kweli naona wanaandamana na hilo neno ndo Rejista inayotumika sana ! Ila sielewi

Kuuliza si ujinga ! Nisanueni
Sheria ya Bajeti. Yetu imepitishwa Jana na nadhani wengi hawajui Kama Jana tumepitisha finance bill ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…