Vijana wa Kiume badilikeni

Mtu anayejitambua aliyeelimika, awezi kuangalia jamii,

Kujikomboa ni pamoja na kukabilianana hizo myth
Wewe unasema tu. Kama hukuwekewa msingi mzuri ni ngumu. Utokee tu ujasiri. Kusingizia elimu sidhani kama ni sahihi. Unadhani wanaofanya kazi mpaka umri wa kustaafu hawapendi kujiajiri..! Au na wao elimu haijawakomboa ...?
 
Tusisingizie sana mtaji.. Kazi kama ya saidia fundi haihitaji mtaji na Kazi kama ya bodaboda pia haihitaji mtaji sababu tajiri atakupa mwenyewe pikipiki kwa mkataba.. Kazi ya kuweka nyimbo kwenye simu na movies mtaji ni kompyuta yako tu na asilimia kubwa vijana humaliza chuo wakiwa na computer so bado hapo point ya mtaji unakuwa ipo kwa mbali sana..

Wakati wewe unatumia hiyo computer kuangalia movie.. kuna mtu anatamani aipate ili afanyie Kazi za graphics, stationery n.k

yani kiukweli mambo ya kufanya ni mengi sema vijana hatujiongezi na hatuji raha ya kujiajiri, sababu hakuna tajiri duniani muajiriwa labda uwe fisadi yani.

Kingine vijana tutumie internet kujifunza new skills.. chuo pekee hakitoshi kutupa kila kitu sababu dunia inabadilika kila kukicha.
 
Mi nadhani tukubali kuna wachache wenye changamoto lakini Kama tukiamua kuwakebehi vijana wa kiume kwa kuwa uchumi wao mbovu hivyo ni wavivu na wazembe tunakosea sana. Ukifanikiwa kupenya usizisahau njia hata kuwasema vibaya ambao hawajafanikiwa

Unaweza kuona anabeti au anacheza gemu au amekaa ukadhani afikiri au haoni hali yake ni mbaya ila kiukweli kwenye maisha kuna mahali inafika haujui hata ukiamka uende wapi au ikifika jioni ni nini utakula bahati mbaya sana hakuna anayejali yeyote unaemueleza anakuona mzembe, Kama wewe ni wamakamo na unavijana wako wanaonesha nia embu washike mkono maana mambo kwa ground usiyaelezee Kama hujayapitia
 
Mkuu wengi hawajitambui wanachagua kazi
 
Huko arusha si nasikiaga kila mtu ni bilionea
 
Sio wanakuona je hawakupi hata hiyo michongo yenyewe mpaka twende sehemu mbali na home ambako hawajui id ya muhusika
 
Bado vijana wanahangaika sana tu ndugu zangu hao wavivu wachache walikuwepo toka zamani tu.
Ila tu ni kua sasa hivi ni kweli wanawake wameamka sana sasa kuamka kwao kunaonesha sasa vijana wa kiume wamelala kitu ambacho si kweli kabisa, wanaume wanapiga kazi mnoo. Ishu ni kua hizo biashara za wanawake nyingi ni za kutembeza na kuonana na watu sana hasa hizo za uchuuzi wa vyakula kula kama mihogo, karanga ,n.k. Nenda kwenye maeneo ya ujenzi wa barabara,nyumba,masoko ya mitumba huko utatukuta wanaume kedekede mkuu, hizo laini laini wacha wafanye muwape promo kama hizi.

Mtoa mada umeongelea mambo ya vikoba na vikundi na mambo kama hayo ambayo mostly yanafanywa ili kumkuza mwanamke ni mara chache sana wanaume kua na vikundi vya namna hii, huenda hata wewe mleta uzi haupo kwenye hivi vikundi. Wanaume wengi sio watu wa vikao vikao sana na kukutana mara kwa mara kama wanawake wanavyofanya kwenye hivyo vikundi vyao, na hii ni kutokana na shughuli zao.

Huyo nduguyo ni mvivu tu na umkanye mara moja cha ajabu hujaleta mrejesho wa jinsi gani unamshughulikia nduguyo badala yake unatuhumu vijana wengine wengi kwa kuwaweka kundi moja na nduguyo (japo wapo lakini sio wengi kama mnavyotuaminisha hapa).

Vijana tuchape kazi dunia imegeuka sasa women empowerment inawezeshwa zaidi na wanaume kama mleta uzi kwa kuleta propaganda za uongo uongo kama hizi.
 

Bora umewachana kweli,,,maana naona watu wanaongea bila kutafuta mizizi ya tatizo,,,best believe hawa vijana sio kwamba wanapenda maisha ya ulofa,,,ni kwamba jamii iliwapeleka mashuleni na kuwajaza fikra kwamba wakikamilisha masomo yao,,watakuwa marketable kwenye fani zao na kuishi maisha mazuri,,,cause ajira zitakuwa zinawasaka,,,,but it turned out to be totally opposite,,na wengi wameangukia kwenye bangi cause ya hiyo frustration...hapa kikubwa ni kuacha kutupiana lawama,,,cause kila mtu kachangia,,kuanzia serikali,,wazazi na jamii kwa ujumla
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daahhh kwahiyo umeona umjibie humu humu
 
Sawa vijana wetu wamekuelewa sana. Ila na vijana wa kike nao inabidi wafundishwe waache tabia za kudanga na kuwa ombaomba. Waambieni wazi kuwa k zao siyo chanzo cha kipato bali ni kwa ajili ya kusaidia kuzaa na kutoa haha ndogo.
 
Nafahamu sio wote wanaobweteka ila unapowahukumu vijana wote basi utakuwa unakosea maana kuna wengine wanahitaji muongozo wa kushikwa mkono, Ngoja nikupe ushuhuda kiufupi.

Mimi hapa, nilianza kazi ya saidia fundi nikiwa ndogo sana, nikaingia kujifunza computer na ufundi wake mtaani nikamaliza . Likatokea zari la mentali Wahindi wakatangaza ajira kwenye machine ya kuprint nikaajiriwa nimefanya nao miaka miwili wakarudi kwao India machine wakamuuzia Mtanzania, huyo ndo akaja kuwa na roho mbaya kama unavyo fahamu Africa people tulivyo, akanidhurumu mshahara wa mwaka mzima, nikaamua kujiengua,

Nikaingia mtaani nikajifunza umeme wa majumbani hapa sasa sikuwa na jina mtaani wala connection nikawa sipati kazi nikaona bola niachane na umeme maana hata mwalimu aliye tufundisha alikuwa na karoho kakuto kuruhusu upate nafasi ya kujitegemea ila uebdelee kuwa mtumwa wake.
Nikaingia kwenye mafunzo ya upakaji wa rangi ambayo yaliletwa na waTuruck,hapa nikaiva nikapata kazi kadhaa ila shida ikaja katika malipo ikawa unalipa pesa ndogo zingine mpaka umalize kazi, ukimaliza kazi nimwendo wa kuzungushana na kudhurumiwa.
kuna ushuhuda mrefu tu natamani nifunguke ila mimi kama mimi katika hari hiyo unadhani nitabaki katika nafasi gani,
mpaka nashindwa nifanye kitu gani, nipo nipo tu ila sio kwa kupenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…