The Lastdream
JF-Expert Member
- Jan 23, 2024
- 1,970
- 4,616
Jamani wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema. Nimeona ndugu yangu Mlundilwa Jr kaandika uzi wake akisema alimwambia dogo atoe elf20 lakini akagoma akasema bora atafute mwanamke aimalizie huko. Sitaki kujua ni stori ya kweli au ni uongo, lakini uhalisia upo hivyo.
Sasa hivi kwa tunaoishi mitaani tunaelewa. Utakuta kijana shule ilimshinda, wazazi walishaongea mpaka wamechoka. Kazi ni kunyoa na kuweka engo kwenye nywele na kupaka mablaki kama waziri fulani katika nchi fulani.
Unajaribu hata kuonyesha upendo kwa madogo mtaani njoo golini nikufindishe jinsi ya kukata viazi vya chipsi anakuja siku ya kwanza ya pili wiki mara humuoni!
Unabaki unashangaa tu anarudi kushinda kwenye saluni kujipaka poda na jioni kwenye madubu baadae anamalizia Kvant huku anacheza mziki wa singeli. Huyo kijana miaka 27 anakimbilia 30 jitu kubwa halijielewi.
Bado kuna tatizo kubwa sana katika jamii yetu. Haswa kwa vijana wakiume ambao sisi ndio mababa wakesho.
Kuna dogo wazazi waliongea mpaka wamechoka peleka shule wapi. Kaishia kuvuta madawa baba kachoka kaenda kumpumzisha jela. Mama yake alipoenda kumuona tumbo la uchungu likamshika mtoto kakonda vbaya sababu amekosa vile vitu wapo mahakamani wanataka kukata rufaa wamtoe.
Vijana tusichague kazi, tuchape kazi. Haya tujiandae kwenda kwenye kuomba maombi ya semina kwa ajili ya uchaguzi mwakani elfu 50 sio ndogo.
Usiku mwema.