Vijana wa siku hizi ni wavivu na wanachagua kazi

Vijana wa siku hizi ni wavivu na wanachagua kazi

Sasa hapo unaniongelea mimi na sio vijana wa sasa kuchagua kazi in comparison na vijana waliopita ? Ni wangapi wametobosa sasa ? Percentage-wise ?

Kitaa maisha magumu watu wanabangaiza..., watu ni madalali katika level tofauti sasa badala ya kuridhika na mediocrity au kila mtu hadi professionals kwenda kwenye siasa ambayo ndio inalipa kwa watu wenye fikra inabidi kujiuliza nini kifanyike na kinachofanyika sasa is not fit for purpose....; Kama ajira kuu hata kwa afya ni hatari (Bodaboda, Wachimbaji wadogo n.k.) jambo ambalo kama taifa tutalipia kwa kutumia pesa kwa ajili ya Healthcare.., utaona kwamba tunataka kutibu symptoms na sio ugonjwa wenyewe....

Na kutokujituma au kukata tamaa kwa vijana wa sasa au kutumbukia kwenye addiction za kamari hakubadilishi statement ya kwamba uchaguzi wa sasa wa kazi between vijana wa sasa na wa zamani does not hold water...
Una andika mambo makubwa kuliko uwezo wake. Unapoteza wako.
 
Jamani wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema. Nimeona ndugu yangu Mlundilwa Jr kaandika uzi wake akisema alimwambia dogo atoe elf20 lakini akagoma akasema bora atafute mwanamke aimalizie huko. Sitaki kujua ni stori ya kweli au ni uongo, lakini uhalisia upo hivyo.

Sasa hivi kwa tunaoishi mitaani tunaelewa. Utakuta kijana shule ilimshinda, wazazi walishaongea mpaka wamechoka. Kazi ni kunyoa na kuweka engo kwenye nywele na kupaka mablaki kama waziri fulani katika nchi fulani.

Unajaribu hata kuonyesha upendo kwa madogo mtaani njoo golini nikufindishe jinsi ya kukata viazi vya chipsi anakuja siku ya kwanza ya pili wiki mara humuoni!

Unabaki unashangaa tu anarudi kushinda kwenye saluni kujipaka poda na jioni kwenye madubu baadae anamalizia Kvant huku anacheza mziki wa singeli. Huyo kijana miaka 27 anakimbilia 30 jitu kubwa halijielewi.

Bado kuna tatizo kubwa sana katika jamii yetu. Haswa kwa vijana wakiume ambao sisi ndio mababa wakesho.

Kuna dogo wazazi waliongea mpaka wamechoka peleka shule wapi. Kaishia kuvuta madawa baba kachoka kaenda kumpumzisha jela. Mama yake alipoenda kumuona tumbo la uchungu likamshika mtoto kakonda vbaya sababu amekosa vile vitu wapo mahakamani wanataka kukata rufaa wamtoe.

Vijana tusichague kazi, tuchape kazi. Haya tujiandae kwenda kwenye kuomba maombi ya semina kwa ajili ya uchaguzi mwakani elfu 50 sio ndogo.

Usiku mwema.
Usilinganishe kizazi hiki na sie wahenga, hiki ni kizazi, kinachotaka Mambo yaende fasts(inawezekana) jamii inawakosea sana vijana wa 1998 kuja juu
 
Unachokisema ni kweli 90% hata hapa nilipo naona wavivu mno wanashinda kwenye pooltable. Ubishoo wa kifala yaani.

Kazi usela mavi na kupiga piga piga vizinga jero buku.
Ukimpa kazi siku ya kwanza ya pili humuoni. Sijui wanadhani maisha ni maigizo kuna miujiza huko mbele.
Hata hao wanaowaiga akina Chinno wanafanya kazi.

Kazi wanazopenda ni zile za kivivu vivu. Kuuza duka la nguo.. kuñyoa saloon basi.
Kuna mmoja mtaani Kila siku alikuwa ananisumbua kuhusu michongo simpi. Siku moja nikamwambia twende shambani kwangu Kuna kazi ya miezi 2 na mshahara laki mbili,kulala na kula juu yangu. Baada ya wiki moja vibarua shambani wakaanza kunipigia simu kwamba dogo kazi yake kutwa ni kucheza Yale mabonanza na kubeti na kulewa. Nikachunguza na kuona kweli, yaani fasta nikamtimua.
 
Kuna mmoja mtaani Kila siku alikuwa ananisumbua kuhusu michongo simpi. Siku moja nikamwambia twende shambani kwangu Kuna kazi ya miezi 2 na mshahara laki mbili,kulala na kula juu yangu. Baada ya wiki moja vibarua shambani wakaanza kunipigia simu kwamba dogo kazi yake kutwa ni kucheza Yale mabonanza na kubeti na kulewa. Nikachunguza na kuona kweli, yaani fasta nikamtimua.
Yaani hawajitambui mkuu coz niko kwenye rika lao nawaona. Yaani wazito wazito...

Unakuta ana uhakika wa kula home na kulala basi.
 
Back
Top Bottom