Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Seydou, say yee, say forever ... kumbe vijana wa zamani (bbc) mko wengi humu JF! Choggy Slay yuko wapi?
 
Enzi hizo ilikua burudani kwa sana yani daah! Watu tulienjoy ujana
 
Daaaah . . . kweli ulikuwa mtu wa viwanja . . . . Hawa walikuwa wanatumbuiza Silent Inn Mwenge au ili ya pale Kimara (Nimesahau jina)
Safari Resort Kimara, and kila Jumatano OSS walikuwa wanapatikana Kinondoni Stereo Bar, nilikuwa sina kiingilio hivyo hukaa nje kusikilizia mambo nje ya Ukumbi
 
Yaweke hadharani mkuu
 
Dah......enzi hizo nikiwa relwe Tabora.......jamaa yangu Filipo akaniacha akahamia RTC Kagera.......kipindi ndio ule wimbo wa Sisily umetoka......acha kabisa......

Umenikumbusha tulipokuwa tunaingia Ochestra Matimila Songea kabla hawajarudi Matimila Bar pale Mwananyala. Kiki na wenzake wakiwa wanapiga Top Life Bar kinondoni! Ilikuwa shida!
 
waigizaji kama fred williamson, jim kelly,mwana dada pam grier,bo sevenson, amita,hema malin,vinod,ponam walikuwa juu, sinema kama black ceaser, three the hardway,enter the dragon,black samurai,amar akbar antony,dilwale,sholay nk.
Bila kumsahau Bruce lee mbabe wa kung fu.
 
Daaaah . . . kweli ulikuwa mtu wa viwanja . . . . Hawa walikuwa wanatumbuiza Silent Inn Mwenge au ili ya pale Kimara (Nimesahau jina)
Kimara white house kama sikosei bila kusahau masantula ngoma ya mpwita.
 
Kwa vijana wa Tanga enzi hizo ni mkonge hotel snack bar kwa dj mansuet au mwambani kwa marehemu dj rujo. Kweli wakati haurudi vijana wa sasa sijui kama wanapata raha kama enzi hizo.
 
Mzee wa fido dido swag nimeingia mambo yeee mambo yege dole tupu bila kucha.
 
Kwa vijana wa Tanga enzi hizo ni mkonge hotel snack bar kwa dj mansuet au mwambani kwa marehemu dj rujo. Kweli wakati haurudi vijana wa sasa sijui kama wanapata raha kama enzi hizo.

Haaaa haaaa umenikumbusha mbali. Kulikuwa na kijana moja mtoto wa Mataka walikuwa na mabasi ya TAMTA alikuwa never miss Mkonge Hotel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…