Sina mambo mengi
Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.
Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.
Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Swali ni kama ifuatavyo. Kwani hapo Rwanda tuu kuna bodaboda kibao tuu kama Tanzania ila mbona wao wana fuata sheria.
Wanavaa helmeti, wana heshimu taa za barabarani kama kusimama, wako na speed nzuri na wanavaa smart kama wanaenda ofisini.
Iko hivi mimi naona Tanzania kitu kinacho itwa Kufuata sheria bila shurti ni kitu kigumu sana. Na hio yote ina tokana na kwamba kama juu viongozi hawafuati sheria ni ngumu sana huku chini sehemu yoyote watu Kufuata Sheria, we elewa ya kwamba tunaishi kwenye nchi moja ambayo watu wake hawajui kujiongoza wala kujisimamia na hili swala la bodaboda lime prove the point.
Kama mkubwa wako hana muda na sheria sasa weww hiyo sheria ina kusaidia nini kuanzia kuijua mpaka kuishi ndani ya sheria.
Nenda Rwanda tuu hapo uone watu walivyo smart, jiji safi, camera kila sehemu...Kagame japo ana changamoto zake ila aliamua kuijenga Rwanda na watu wamekubali Kufuata sheria na kuijenga nchi yao.
Jiji safi,camera kibao, barabara nzuri zenye ubora, ...... Mimi ninasema siku zote Tanzania sisi bado sanaaaa...hapa ni ulaji tuu hakuna kujenga nchi wala nini na kila sehemu ni danganya toto viongozi wana piga hela wanapita kushoto mwananchi uta jijua mwenyewe.