Vijana wanakufa kwa ajali za bodaboda kila siku. Serikali haina taarifa au kwakuwa wahanga ni familia za kimaskini?

Vijana wanakufa kwa ajali za bodaboda kila siku. Serikali haina taarifa au kwakuwa wahanga ni familia za kimaskini?

Inatakiwa ifanye jambo la busara kuwaokoa hawa vijana. No jambo Gani la busara, kazi kwao..!
Mtu anakataa helmet, side mirror, anabeba mishkaki, hazingatii traffic lights, anachoma mabasi, anabeba mkaa gunia 8 kubwa

Wewe traffic polisi pekeyako utamuweza ?
 
Sina mambo mengi

Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.

Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.

Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Waziri kangi lugola alisema boda boda waachwe hata wapakie watu 10 sawa tu
 
FB_IMG_1709780303279.jpg
 
Serikali itumie sheria za usalama barabalani mbona ziko wazi tu
Kuna siku nimesimamishwa na matrafiki barabarani kwa kuzidisha mwendo. Sasa wakati nawapiga "sound" wanipunguzie adhabu kutoka 30,000 hadi 2,000, wakapita jamaa wa bodaboda wako spidi balaa na hawana helmet wala nini..

Nikamuuliza yule trafiki ni kwanini hawawakamati hao bodaboda ilhali wanavunja sheria waziwazi?

Jamaa akanijibu "bro, hivi we unavyowaona hao walivyo spidi nikiwasimamisha watasimama? Au ndio ntawasababisha waanguke kabisa? Na je wasiposimama unataka mimi mtu na akili zangu nianze kukimbizana na hao "wehu"?

Nikamuelewa.
 
Sina mambo mengi

Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.

Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.

Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Swali ni kama ifuatavyo. Kwani hapo Rwanda tuu kuna bodaboda kibao tuu kama Tanzania ila mbona wao wana fuata sheria.
Wanavaa helmeti, wana heshimu taa za barabarani kama kusimama, wako na speed nzuri na wanavaa smart kama wanaenda ofisini.
Iko hivi mimi naona Tanzania kitu kinacho itwa Kufuata sheria bila shurti ni kitu kigumu sana. Na hio yote ina tokana na kwamba kama juu viongozi hawafuati sheria ni ngumu sana huku chini sehemu yoyote watu Kufuata Sheria, we elewa ya kwamba tunaishi kwenye nchi moja ambayo watu wake hawajui kujiongoza wala kujisimamia na hili swala la bodaboda lime prove the point.

Kama mkubwa wako hana muda na sheria sasa weww hiyo sheria ina kusaidia nini kuanzia kuijua mpaka kuishi ndani ya sheria.

Nenda Rwanda tuu hapo uone watu walivyo smart, jiji safi, camera kila sehemu...Kagame japo ana changamoto zake ila aliamua kuijenga Rwanda na watu wamekubali Kufuata sheria na kuijenga nchi yao.

Jiji safi,camera kibao, barabara nzuri zenye ubora, ...... Mimi ninasema siku zote Tanzania sisi bado sanaaaa...hapa ni ulaji tuu hakuna kujenga nchi wala nini na kila sehemu ni danganya toto viongozi wana piga hela wanapita kushoto mwananchi uta jijua mwenyewe.
 
Sina mambo mengi

Hali ni ngumu, kila siku unasikia misiba huku na kule.

Nazungumzia hii misiba ya bodaboda, serikali iko kimya kama hamna kinachoendelea.

Je, serikali haina taarifa ya misiba hii ya bodaboda au haijali kwakuwa wahanga ni familia maskini?
Wahanga kwa kuwa ni familia za......
 
Safety starts with you,dare to be aware,ride safely and do right things even no one is watching you,do what is right not what is easy,

When u gamble with safety,you bet your life.
 
Boda boda akili hawana yawezekana hata wengi wanaopanda boda boda akili hawana....

Unataka serikali ifanyeje sheikh?
 
Back
Top Bottom