Kuna mambo makubwa kama mawili au matatu lazima uyafanye.
1. Jiandae kifikra kabla hujaachaa (mental preparation), hichi kitu muhimu sana na kinaweza chukua muda sana. Sababu kwenye kitu chochote psychology inachukua nafasi kubwa sana. Muhimu hapa ni kwamba hakikisha unafikiria positive side na unakaa mbali na negative thinking, sisemi uwe naive maana kuna tofauti kubwa ya kufikiria positive na kuwa naive. Andaa kichwa chako kupambana na "naysayers" wazee wa kukwambia utashindwa, huwezi kufanikiwa, utajuta, utasaga na ndala. Hawa lazima ujue jinsi ya kufanya fikra zao zisiingilie fikra zako, lakini kujiandaa kifikra ni pamoja na kuandaa kuishinda sauti ya ndani (inner voice) ambayo inakuongelesha kwa ndani kukwambia unajua mkuu ukichemka hapa familia yote choka, au at least wewe unapata 700,000 kwa mwezi, wenzio wanapata 0. Hii ikatae kabisa, kwa kujiandaa kifikra. Sikiliza sana motivational speakers kwenye youtube kama kina Les Brown, Napoleon kwa Tanzania kina Erik Shigongo, Mr Mauki na wengine.
2. Andaa Plan nzima ya mchezo kwenye karatasi. Najua watu wengi wanasema nisha plan, kila kitu na plan yenyewe kwa bahati mbaya ipo kichwani. Hawa wanajindanganya tuu. Plan lazima iwe kwenye karatasi, iweke uione na ujinasabishe nayo. Isome mara kwa mara rekebisha sehemu zinazo stahiki. Ibandike kwenye kuta za chumba chako, isome na ujirecord kisha isikilize over and over ukiifanyia maboresho. Mfano, unataka kufungua supermarket ndogo plan lazima iseme wapi, ukubwa wa duka, mtaji, njia yako ya kufanya marketing na kupata masoko. Plan ndio ushindi, mechi haishindwi uwanjani mechi yoyote inashindwa kwenye plan. Kama Plan zako ni weak, jiandae kuondolewa kwenye reli.
3. Test plan yako hapo juu kwa kufanya uchunguzi.Hii ni pilot process, unaweza kutembelea wenye hiyo biashara ukaangalia na kujifunza, unaweza kuanza kidogo. Hapa nafasi ni kubwa inategemea wewe unataka kutest vipi plan yako.
4. Never have Plan B. Usisubutu kuwa na Plan B, sababu plan B inaairibia Plan A tuu hakuna jingine. Ukipigana na mlango wazi ni tofauti sana kupigana mlango ukiwa umefungwa.
5. Never regret ukijaribu. Mimi nilipakiza watoto na familia kwenye ndege kurudi Tanzania baada ya miaka 15 ughaibuni na nilikuwa na maisha standard kabisa. Kikubwa nilichoshinda ni kwamba niliapa kuto kujilaumu kwa maamuzi niliyofanya. Life is too short kutojaribu roho nini inataka.
I support yoyote anaetaka kuacha kazi sababu hao ndio wajenga ajira za wengine wengi ambao mungu ajawapa utashi wa kujiamini na kufanya maamuzi magumu.