Mkuu naona una negativity sana anyway, ni mawazo yako na ninayaheshimu.
Kwa mtazamo wa hapo juu, watoto wa wazazi wasiosoma hawatasoma kamwe kwa kuwa mzazi wake atamwambiaje yeye asome, apende shule wakati mzazi mwenyewe alikimbia umande?
Na watoto Wa masikini hawatakiwi Kusikiliza ushauri wa wazazi wao kuhusu namna ya kupata mafanikio ya maisha kiuchumi.
Mfano, Mzazi wangu sio tajiri lakini kupitia makosa aliyofanya nyuma, anaweza nipa mbinu nzuri za kutusua kimaisha. Mfano yeye awe masikini akinieleza namna yeye alivyoishia kwenye umasikini, mimi nikifanya kinyume cha yeye alivyoishi je?
Mwisho wa siku kuna cynics katika Maisha, ambao watakuambia, hili haliwezekani, mbona flani alifanya akashindwa, kufanya hivyo si raisi, kwa mtaji huo huwezi n.k. Hizo ni kelele, na hiyo ndio sababu kubwa kwanini matajiri duniani ni wachache, chini ya 10%. Hawa ni watu ambao hapo nyuma walichekwa, walitukanwa, walidhihakiwa.
Lakini pia kama mtu anaona asichukue nondo za motivational speakers, achukue basi motivational speakers ambao pia wamefanya makubwa. Hapa Tanzania, soma historia ya Mengi, Bakhresa, MO dewji na wengine utaona wametoka wapi. Nje kuna kiyosaki, Sanders, Glazer, Warren Buffet n.k