Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

At least JF imeanza kurudi kwenye heshima yake. People discuss ideas. Huu uzi kwa sasa ni wa mwaka kwangu. Yale mambo ohhh mara kibamia mara nimeachwa naomba ushauri blablaaaaa yalikuwa hayana positive impact both physically and mentally as well.
Nadhan waanzilishi wa jf wanafahamu huo utofauti wa mawazo na interest za watu ndio maana kukawepo na majukwaa mbalimbali kulingana na agenda.
 
Mkuu umenitia moyo sana nmepanga baada ya mwaka niache kazi nijiajiri,Jana nilikuwa naongea na aunt yangu alinikatisha tamaa sana akasema mwanang sikushauri uache kazi kabisaaa,km umeamua kufanya biashara fungua asimamie mwingine uendelee na kazi
Lkn kazi yangu inachosha nafanya kazi na matusi juu,kuna wakati nalia
Kwa hili andiko lako limenitia moyo
Kwa nia thabiti nitaweza
 
Hahahahahaa uwekeze milioni Halafu mtu akuzalishie? Danganywa, nimeshapoteza saaana aiseee
 
Tanx mkuu
 
Asante sana mdau, utajiri wa kwana ni kuwa na mfumo wa biashara na sio mtaji tu, kuna watu wanayo mapesa lakini hawajui cha kufanyia. Ukiwa kaini ni rahisi kujaribu MAMBO mbalimbali ili kujitafutia mfumo wako pekee wa kukuingizia kipato, ni nadra sana kupata mfumo sahihi kwa jaribio la kwanza, hivyo basi ukiwa kazini ni unakuwa na ujasiri wa kujaribu mambo mengi bila woga na hatimae utajipatia system uipendayo kisha fanya maamuzi ya kuacha kazi ili ukauendeshe mfumo wako kikamilifu. Usiache kai eti kwakuwa unamtaji no hakikisha unajua unaenda kufanyia nini mtaji huo.
 
Jambo ambalo siku zote naliamini kwa asilimia nyingi katika maamuzi yoyote unayotaka kuyafanya ni USIRI wa kitu unachotaka kukifanya au kuja kukifanya,kama unampango wa kuacha kazi Hilo ni wazo lako na hakikisha kuwa N lako peke ako kwan ukiamua kumshirikisha mtu mwingine kuna mawili 1.akusapoti 2.akukatishe tamaa.

Kwa kua hatuna uhakika na tutakao washirikisha mawazo yetu bhas hatuna budi kubaki na mawazo yetu wenyewe,sasa basi kwa kua unampango wa kuacha kazi naamini tayari kichwani mwako umeshajua na kupanga kazi gani utaifanya baada ya kuacha hiyo kazi,kinachofuata sasa baada ya kujua kazi unayotaka kuja kuifanya baada ya kuacha hiyo ya utumwa.

Ni kuyatoa mawazo yako nnje kwa watu sahihi,watu sahihi ni kina nani hapa? Watu sahihi ni wale watu wanaofanya biashara ambayo unataka kuja kuifanya baada ya kuacha kazi...na sio Kila mfanyabiashara kwa mfano: unataka kuja kufungua saloon ya kike/ya kiume watu sahihi wa kuomba na kuwashirikisha mawazo yako ni mtu alie na saluni yake Huyo ndie atakututia moyo,atakwambia magumu,atakwambia faida,hasara,changamoto nk Lakini kamwe hatokushauri usifungue zaidi zaidi atakupa mbinu za kufanya ili biashara yako isiwe ngumu.

Lakini kamwe na Usije jaribu kufanya makosa kuomba ushauri wa biashara yako ya saluni(mfano) kwa mtu anaefanya biashara ya kuuza simu,kuuza duka,kuuza nguo,nk nk... kwani hata siku moja mtu anaefanya biashara baki hana idea na biashara yako so atakupa majibu ya juu juu kutokana na anavyosikiaga na zaid atakukatsha tamaaa na mwisho atakuaminisha kua Biashara yake ndio bora kuliko hiyo unayotaka kuifanya wewe.

Sasa Basi kwa kua umeshadhamiria kuja kuacha kazi TUNZA SIRI yako halafu anza kutafuta Watu sahihi wakuwashirikisha siri yako ili ije kua ya maana...Usije omba ushauri ndugu,rafiki au yeyote asie husika na hicho unachokuja kutaka kukifanya kwani Tambua hawana idea na chochote ktk hilo so watakupa majibu ya juu juu na kujifanya wao ndio wahenga na mwisho wakiona unawabishia watakwambia (asie sikia la mkuu.....)

Usikubali kuruhusu upenyo wa mtu baki kukukatisha tamaaa,Fanya,Anza na badae waje wakukute upo unafanya kazi yako hapo ndio utajua yupi alikua sahihi na yupi hakua sahihi kulingana na comment watazokupa baada ya kukukuta kwa mara ya kwanza ukiwa katika biashara yako.

MABADILIKO NI WEWE BINAFSI NA SI MTU WA PEMBENI
 
Kuacha kazi ni moja ya maamuzi màgumu ambayo yanahitaji ujasiri ña mentally preparation. Huhitaji kuwa na kiasi fulani cha pesa ili uache kazi ila unahitaji malengo,kwanini naacha kazi?unataka kufika wapi baada ya muda fulani?unataka uwe una earn kiasi gani cha pesa per month?Hàyo ni baadhi ya maswali yanayoweza kukuongoza kuchora ideas.Mwanafalsa John luis Bragos anasema"if you want to think more creative,you must challenge the boundary".Ukiwa unajiandaa kuacha kazi lazima ubadili mfumo mzima wa maisha wakati mwingine hata marafiki(mates)wako ili kuweza kufikiri out side of the room.A real estate investor Sir Donald Trump said"You have to think anyway,so why don't think big"Lazima uwe na malengo yako ya muda mrefu na uchore mpango kazi namna ya kuyatimiza hayo malengo.
Ukiongozwa na msukumo wa ndani na ukajifunza kwa waliofanya wakafanikiwa(mentor) naamini itakupa mwanga mkubwa sana katika safari Yoko.Note usiombe ushauri kwa wafanyakazi wenzako watakukatisha tamaa na kukutia woga.

Binafsi ni mwajiriwa but nimeweka malengo kuwa ikifika 2025 nataka kuacha kazi kwani nimeajiriwa 2015.Kwa kuwa safari yeyote inahitaji maandalizi nilishaanza kujiandaa since day one naingia kazini.Nasoma vitabu kwa wingi kuongeza maarifa lakini natafuta taarifa kwa hali na mali lakini pia nimeanzisha project ambazo zinanisaidia kuniongezea uzoefu katika kujiajiri.
My take.Failure is party of process of success
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…