Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

mi niliajiriwa kwasasa nimejiajiri

Wakati naacha kazi nilichukulia kama dharura
 
Hii kweli kabisa
 
Hii tunaita kwenda sio tatizo tatizo ni kupata ulicho kiendea
 
Mkuu mkuu mi sio msomaji wa vitabu kama unavyo hisi mi ni moja ya watu walio jiajiri kwa mtaji mdogo mpaka kufikia kumiliki biashara ya uhakika japo kwa sasa upepo umeyumba
 
Ujanja ni kujiajiri kwa asilimia 90 halafu ukaajiriwa kwa asilimia 10 tu ili uwe unapata mkopo na kuufanya kama mtaji kwa kujiajiri!!!
Wengi waliofanikiwa kwa viwango vya juu niliwaona wanatumia hii staili.
Anakwenda kazini kuripoti tu lkn concentration yake ipo kwenye biashara yake.
Lkn hii inawezekana endapo majukumu yako ya kazini ulipoajiriwa hayakubani sana.
But ni ngumu sana Kama ukienda kazini ulipoajiriwa unakuwa bize kwa masaa 12.
 
Kuna mbinu nyingi za kujifunza kujiari unaweza ukawa bize na ukawa bado unafanya biashara
 
Kuna mbinu nyingi za kujifunza kujiari unaweza ukawa bize na ukawa bado unafanya biashara
Ni kweli but inategemea na nature ya business.
Assume biashara yako ni ya kuchukua magunia ya mkaa Bagamoyo na kuyaleta mjini halaf kazini kwako ni Posta/Kkoo na unamaliza kazi saa 12 jioni,utawezaje kutoka town muda huo uanze kwenda Bagamoyo ukachukue magunia ya mkaa.
 
Huwezi ila biashara kufanyika inawezekana

Ndio maana biashara ni mnyororo

Mwanzo unaweza kwenda kuchukua mzigo siku za off au weekend

Na awamu zinazo fuata unatumiwa mazigo

Na ukiona biashara inaenda vizuri ndio unakuja na wazo la kuacha kazi ili uisimamie kwa ukamilifu
 
Sawa umeeleweka.
Ingawa Kuna watu wamelizwa sana pesa zao kwa kuamini huo mnyororo wabongo hawana asili ya uaminifu kwenye mambo ya biashara.
 
Kuna tofauti kati ya self-employment na creating a business. Kama ni biashara, manake inabidi uajiri mt wa kubeba hayo magunia. Wewe kazi yako ni kutafuta clients, kutafuta supplier mwente mkaa mzuri wa bei nzuri, na kuhakikisha operations zinaleta faida nzuri. Lakini ukiongelea wewe kwenda kuchukua mkaa, manake ni self-employment na hiyo ni ngumu kama mtu una kazi. Itabidi uifanye siku ambazo uko off ajirani
 
Ujumbe sahihi huu
 
Sawa umeeleweka.
Ingawa Kuna watu wamelizwa sana pesa zao kwa kuamini huo mnyororo wabongo hawana asili ya uaminifu kwenye mambo ya biashara.
Ni kweli kabisa. Japo pia, kuna waaminifu. Mimi nikigundua mfanyakazi ana uswahili nafukuza hapo hapo. Nimegundua waaminifu wapo, lakini inabidi kuwatafuta na pia NI MUHIMU KUMJALI SANA ILI AONE KWAMBA ANAHESHIMIKA NA ANAPENDWA NA ANAJALIWA NA BOSS WAKE. Na atafanya kazi kwa moyo na uaminifu.
 
Hii kweli waminifu wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…