Kwanza kujiajiri ni process, sio tu kijana aseme sawa nataka kujiajiri kuna mambo ya kuzingatia. Unataka kujiajiri katika nn je hicho kitu umekifanyia research vya kutosha? Ila yote kwa yote Nashukuru Mungu nimeyashinda yote na bado napambana, nimejiajiri katika lishe nauza vijazi lishe kwa watu wowote wenye magonjwa mbali mbali hata kwa mtu wa kawaida tu kupata kinga mwilini. Vijazi lishe vilivyotengenezewa maalum na vyakula ambavyo hatuvili katika lishe yetu na hata kama tunakula tunakula kwa asilimia ndogo sana mfano tre en en mchanganyiko wa kiini cha nafaka kamili, hii husaidia kufungua chembe hai, yani ukinywa tre en en kila siku ni una gurantee ya kutotumia painkillers zozote na afya yako itakuwa zuri sana
Changamoto kubwa kwangu bado nina safari kubwa ya kuelimisha watu umuhimu wa vijazi lishe maana hizi mambo ni utaratibu wa watu wa nje huko, hapa africa hasa tanzania ni kumekuja hivi karibuni tu. Ila kiukweli unywaji wa dawa sio rafiki sana maana dawa ni sumu. Huwezi kunywa dawa wakati hujarekebisha chembe hai yako so its a little bit challenging but nafurahi watanzania tunaelimika kila siku na vinawasaidia watu wengi sana
Rai yangu, kujiajiri ni kuzuri sana na vijana tujaribu kutumia platform kama hizi jamii forum facebook instagram na zingine yani kiujumla mass medias kwa manufaa zaidi. Hakikisha ile vocha uliyotumia imekulipaje katika ujasiriamali wako. Na nahisi tunahitaji group la whatsapp la vijana tuelimishane zaidi na kushirikishana katika fursa mbali mbali