Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Asante sana. Wengi tafsiri ya misemo kama "Usione vyaelea, vimeundwa" ni kwenye mahaba tu.

Hawajui Jamii forum ilianzaje, facebook ilianzaje, wakina Bakhresa walianzaje.

Maswala ya zali za menteli ziliishia kwenye nyimbo ya Profesa J miaka ileee.

Critical thinking inahitajika miaka hii.
 
Asante sana kwa wazo zuri!
Asante kaka. Yaani ni vitu simple sana. SUA vijana wana maliza chuo kila mwaka, wana pambana kusubiri ajira.

Wakati mtaani kuna watu wanaanza biashara za kuku na wanakufa sana kwa kukosa wataalamu wa kuwapa ushauri.

Yeye mtaalamu, kajifungia ndani anasubiri nafasi za ajira Wizara ya Kilimo.

Basi ukiwa unasubiri, kuwa mshauri basi kwa wafugaji kuku au ng'ombe au wakulima.

Lakini vilevile, lazima kuwe na sehemu utakayo patikani, watu hawawezi kukupata chumbani. Ingia ajiras.com weka kuwa unatoa ushauri wa ufugaji.

Asante kaka kwa support yako. Hope tutaweza elimisha vijana wengi.
 
Hivi wale ma modal wanaotokea kwenye matangazo ya tv, mabango barabarani au kwenye social media wanapatikana wapi?

Kwanini usipige picha zako kadhaa, ukajinadi kuwa unaweza kuwa modal kwenye matangazo?

Au kuwa video Queen?

Mfano: Mimi nafanya kazi za social media marketing ya kampuni mbalimbali hapa Tanzania, pia natengeneza matangazo ya platform zetu.

Katika vitu viguma hapa bongo, ni kupata wadada au kaka wakuwatumia kwenye matangazo.

Matokeo yake, tuna nunua picha kwenye mitandao ya wenzutu, wakati Tanzania warembo wapo.

Jamani, tufanye mambo. Hizo picha nilizotumia kwenye hayo matangazo hapo chini nimenunua mtandaoni kwa wenzetu huko. Ina maana hutuna warembo Tanzania?

Sasa hatuwezi kukupata bila kujinadi. register www.ajiras.com post kuwa unaweza pose for ads photographs.

Ndio fursa zenyewe hizi.

 
Habari wana JF,

Hivi sasa kumekuwa na wimbi kubwa la kukosa kazi kwa wasomi wa elimu ya juu mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Mbaya zaidi hata zile shahada ambazo zilikuwa zikitarajiwa kuwa na uhakika wa ajira kama UALIMU, UHANDISI, UDAKTARI na zinginezo nayo pia hivi sasa ni tia maji tia maji kwenye suala la kuajiriwa.

Hivyo inapelekea watu kulalamika sana kuhusu kupata ajira na mafanikio ya wasomi wa hivi sasa.

Hata pia ukigusia suala la kusema muhitimu au msomi ajiajiri, Msomi huyo anapinga au anaona inakua vigumu kwa hoja kuu mbili:

I. Hoja ya kwanza anasema hana mtaji

II. Hoja ya pili ni kuwa mtu ukijiajiri ni lazima uanzie chini kabisa, hapa sasa ndio anakuja na kusema ile elimu aliyosoma miaka yote zaidi ya kumi, ilikuwa na maana gani kwake?

Kwa hiyo tunabaki tu hapo hapo kulaumu kuwa hakuna ajira na hatuna mitaji ya kujiajiri.

Muhimu ni kwamba hatuwezi kuwa tunalaumu maisha yote tu bila kuchukua hatua juu ya hili.

NINI KIFANYIKE
Ni wakati sasa kila kijana kuweka mpango wa kujiajiri mwenyewe tokea anapoingia chuoni mwaka wa kwanza ili kutatua hali hii ya kukosa ajira.

KIVIPI ?
1. Kwa mfano ikiwa labda wewe unasomea uwalimu i.e BA (Education), Bed (com), Bsc (Ed), Bed (Science) nk.

Embu jiwekee mazingira ya kuchonga na kuhifadhi ubao wa kufundishia tokea ukiwa chuoni.

Kisha jiwekee mazingira ya kuchonga angalau mabenchi au madawati manne au matano.

Pia hakikisha vitabu vyako wala huvigawi
Mara ukimaliza chuo tu, basi anza kufundisha angalau TUITUIN CENTER AU NURSERY hapo uwani kwenu pindi unaendelea kuzungusha bahasha, anza hata kufundisha kwa bei nafuu sana au hata tu kwa free offer, hii itakulipa baada ya muda mbeleni

2. Kwa mfano labda wewe umesoma BSC (MECHANICAL) jitahidi angalau baada ya kumaliza chuo tafuta hata ki garage chochote tu hapo.

Anza kufanya kazi hata kwa kujitolea na wala usijali kuwa wewe ni professional engineer na unafanya kazi za technician ila muda huo unaendelea kuzungusha bahasha lakini pia una ongeza mtandao wa kibiashara na kujuana na watu

3. Kwa mfano labda unasoma masoma ya biashara, anza hata kusajili business name yako Brela na kuanza kufanya hata hizi biashara za mtandao ukiwa chuoni wala usijali, tengeneza network ya wateja na ongeza wateja polepole kwa muda wako wa ziada, angalau utakua umepata pa kuanzia

4. Siwezi nikaelezea kila Professional hapa, lakini kwa kila chochote unachosomea ukiwa chuo anza kukitengeneza taratibu ukiwa chuo ili kije kukuajiri au kukuonyesha njia ya ajira hapo baadae.

Kwa wewe ambae umemaliza chuo na umeshakutana na mtanange wa kukosa ajira tayari, hujachelewa anza kujijenga taratibu kwa hatua hizo au tumia kipaji chako ulichonacho nje ya elimu yako na ujuzi wako kwa ajira.

Maoni yangu ni hayo kwa hili dimbwi kubwa la kukosa ajira.

Wadau karibuni kwa kuongezea na kutoa maoni zaidi.

Angalau mtu akipinga au kubishia mawazo haya basi aje na suluhisho mbadala, sio kupinga tu bila kuwa na suluhisho mbadala.

Karibuni
 
Kichwa yako ni suri.Uko sawa kabisa!
 
"Hakuna chuo kinachofundisha kujiajiri au kuajiriwa"

Kila taaluma inakupa mbinu, ujuzi na maarifa ya kukuwezesha kuimudu na kuiendeleza taaluma husika isipokuwa kujiajiri au kuajiriwa ni maamuzi tu.
 

Maoni maridhawa.

Binafsi hupenda kuwashauri vijana kusoma kitabu kiitwacho Mastery kilichoandikwa na Robert Greene. Hapo vijana huweza kufanya maamuzi yatokanayo na taarifa, juu ya namna bora ya kujiendelea kitaalam na kitaaluma.
 
KILICHOTOKEA MPAKA KUFIKIA HAPO
1. Hoja ya kwanza "Sina mtaji"
Hoja hii imetokana na mambo yafuatayo;

a. Elimu aliyofundishwa huyo mtu tangu mdogo, aliyoyaona wazazi wake wanafanya, walimu waliomfundisha kwa zaidi ya miongo kadhaa ni kuwa "tegemezi". Kajifunza kuwa yeye hawezi kuwa na wazo na akalisimamia mwenyewe mpaka awepo mtu wa kumsukuma 'Mwajiri'.

b. Ana amini kuwa uwezo wa nje 'pesa' ndo una tafsiri utu wa mtu. Si kweli; ukitaka kuamini, mfilisi Mo*** au yule mwenzake Bakh*** waanze kwenye zero kabisaa kama wewe unayesema huna kitu; tuje tuwapime baada ya miaka 10, je, mtakuwa sawa? Kama una uhakika kuwa mtakuwa sawa basi kweli tatizo ni pesa, lakini uki-reason kuwa hamtaweza kuwa sawa basi ujue sababu ya hivyo ulivyo siyo pesa but something else!
Angalizo kwa wazazi; " Acheni kutufanya wanenu Human things, Tunaomba mtulee kama Mungu alivyotuumba Human beings"
-Mtoto atakuwa na degree au P.h.d lakini ataona hawezi kufanya chochote kwa sababu hana (Things: pesa, gari, somebody n.k)
-Mnafikiri wimbi la wapiga mizinga under 25 linalozungumzwa na kulalamikiwa huko mtaani limetokea wapi kama siyo hao tuliowalea kama Human things? Yeah they have education, and a lot of energy, but They need things!

2. Hoja ya pili; "Kuanza chini, mmmmh! Maana ya kukaaa darasani ilikuwa nini?"
Hoja hii inatokana na yafuatayo;

a. Uoga wa "nitaonekanaje kwa jamii inayonizunguka?" Ndg waalimu huko mashuleni, mtoto alikuwa akifeli, mnamfanya afeel au aone kuwa kufeli ni kitu kibaya sana.
Si kweli kuwa kufeli ni jambo baya, bali ni sehemu ya kujifunza, utajifunzaje kama hakuna makosa? Na shuleni nimekuja kufanya nini mpaka mnanifanya nione kuwa "perfect" ndo kujifunza khaaaa! Kama niko perfect nisingekuja kupanguswa kamasi class kwako. Mtoto wa mwenzio akikosa swali, acha kumkashifu, kumzomea na kumtenga hadi stream! Jamani!

Hiyo mentality ya (nitonekanaje) imetokea hapo, mtu wa hovyo ni yule aliyefeli, au mtu wa chini ni yule ambaye hakwenda shule. Mmewadanganya watoto wa watu na vi- stream vyenu weee, na vimaksi na viripoti vya nani kawa wa kwanza na ni nani kawa wa mwisho, matokeo yake ndo hayoooo! Wanaamini kuwa aliyefaulu ataenda mbele na kupata ajira mapemaaa! Haya sasa yuko mtaani.

NDUGU MHITIMU ZINGATIA HILI LITAKUSAIDIA; ukweli ni kwamba "Huko shuleni wenzako tulikuwa tunanoa shoka vizuri, ili ukifika muda wa kukata miti (mti wa umaskini, mti wa ujinga na mingineyo) shoka lisitusumbue kwa sababu ni butu.

Hayo mashoka unayoyaona mtaani na unahisi " they don't make any progress, look at them, i went to school and now I'm back, what have they done?"
Ni kwa sababu hayako sharp, au pengine hayafahamu wajibu wao. Lakini wewe mwenzetu tayari umenolewa hebu anza kuonesha ufanisi wako, ili na wale wenzako ambao hawakujaaliwa kupata kauwezo kama kako, waone kwa vitendo. "The way you take thing's from zero to hero"

Jamaani! Umefika uwanja wa kazi unauliza 'miti ilokatwa iko wapi?' Wakati sisi tunakusubiri wewe ndo utoneshe wenzio jinsi ya kuiangusha hiyo mipingo?

b. Watoto wengi wanasomea vitu wasivyovipenda, kamwona mjomba mwalimu anafundisha baasi naye anataka kuwa mwalimu, kasikia shangazi kawa engineer basi naye anataka.
Siyo hivyo tu; ndugu, Jamaa, wazazi na marafiki walipiga debe kweli kweli; "Acha ujinga wewe, somea kitu fulani kwani humuoni fulani?"
A problem!
Huwezi kumlazimisha mtu kama huyo a "start small". Hana passion, hana purpose hana dream na hicho alichosomea, anachotaka pesa tu. Unaona madhara ya kulea "HUMAN THINGS?"
 
Umetisha, ngoja nifatilie kitambulisho cha Magufuli maana mtendaji ananichelewesha.
 
Michango na mada ama hizi zinanifanya niwaambie madogo kama wakiwa wavivu kusoma vitabu basi waisome JF
 
Emperor Epiphany yani umemaliza kila kitu, nashindwa na sioni cha kuongeza juu ya haya maelezo yako,
Vizuri
 
Utunzi wa comment yako hii inatakiwa kufunguliwa uzi hapa JF ili vijana wajifunze zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…