Jane Msowoya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2017
- 4,302
- 7,815
Yes, ila ngoja ntawaadisia siku mojaPole kwa changamoto ulizokutana nazo. Unaweza kutupa uzoefu wako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes, ila ngoja ntawaadisia siku mojaPole kwa changamoto ulizokutana nazo. Unaweza kutupa uzoefu wako
Anaitwa David stevensonJe unakumbuka jina la Author
Duuuhaisee bora muachie wengine kwa sababu mmeshakula sana huko serikalini.
Ujue tajiri anae ajiri watu wale watu wanamsaidia kutimiza ndoto zake za kuwa tajiri na wale waajiriwa wanakuwa wanapambana na mkate wa kila siku ila uhai wao uwepoUzi mzuri coz hakuna tajiri mwajiriwa Bali kuna tajir anaeajir watu
Good idea lakin mziki wake mhHeshima kwenu viongozi
Nimeona ni vyema na sisi wenye lengo la kuacha kazi tukawa na uzi wetu kama wenye agenda nyingine walivyoanzisha uwanja wao.
Lengo la nyuzi hii ni kupeana mawazo, moyo na uzoefu wa mbinu bora tunazotumia katika maandalizi yetu ya kuachana na aina Mpya ya utumwa, yaani KUAJIRIWA.
Lengo lingine la uzi huu ni kuonesha sababu ya uamuzi wa kutaka kuacha kazi ili kila mtu apime kama sababu yake ni sababu tosha ya kufanya hivyo ama la, lakini hii pia inatoa fursa kwa wachangiaji wengine kufanya assessment ya maamuzi hayo.
Kuacha kazi na kujiajiri na pengine baadae kufikia hatua ya kuajiri ni uamuzi wa kuyatoa maisha yako mikononi mwa mtu mwingine (muajiri) na kuyakabidhi mikononi mwako mwenyewe. Ni kujitoa katika kutawaliwa na kuamua kujitawala mwenyewe. Ni vyema pia tukajulishana gharama za maamuzi hayo mazito ya kutoka Misri kuelekea Kanani. NI WAZI HAITAKUWA SAFARI NYEPESI.
Tushauriane time scale, mfano mimi ninakimbizana na miaka Mitatu kabla sijatoka kwenye hii Jela. Baada ya hapo ntarudi uraiani, nyumbani kuishi maisha yangu ya uhuru.
Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.
Kila mtu anaweza kuwa na sababu yake ya kuacha kazi. Wengine watakwambia kazini kipato kidogo, lakini amini nakwambia hata ukiajiri na kutoweka mwili, moyo na roho yako kwenye hiyo kazi, unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata kile cha kazini. Katika swala la kipato, tofauti ya kipato cha kuajiriwa na kujiajiri ni kipato kimoja Anapanga mtu akulipe kiasi gani, na Kingine Unapanga wewe uingize kiasi gani.
Wengine watakwambia, wanataka waache kazi sababu ya Mateso kazini,ubabe wa mwajiri, kutojali kwa mwajiri. Yote hayo yanakupa HASIRA, geuza hasira zako kuwa DRIVES, zigeuze kuwa USONGO.
Kwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi. Sitaki kumpigia mtu mmoja Magoti (bosi) ili kipato changu kiendelea kutiririka. Bora nipigie magoti watu wengi (wateja) ili kipato kiingie, kwani mteja mmoja akiamua kunifukuza kazi ntakuwa na option kwa mteja mwingine.
Uzi wetu TUNAOPANGA KUACHA KAZI, the clock is clicking....LET'S DO IT, LET'S GO.... Tunapenda pia kuchota busara za wale walioacha kazi na wapo wanaendelea kupambana.
Inawezekana, iwapo mtu utajipanga vyema. Hasa hasa baada ya kuhakikisha mzunguko wako wa fedha uko imara kulingana na vitega uchumi ulivyo jiwekea.Good idea lakin mziki wake mh
Mkuu ni kweli mziki wake ni mnene. Imagine sasa hivi ukivyoajiriwa ukichalewa kutofika kazini mwisho wa mwezi mshahara upo pale pale, lakini ukichelewa au kutofika kazini kwenye kazi yako mwenyewe ina maana tayari pato ulilotarajia kulipata limeshapungua.Good idea lakin mziki wake mh
KweliMkuu ni kweli mziki wake ni mnene. Imagine sasa hivi ukivyoajiriwa ukichalewa kutofika kazini mwisho wa mwezi mshahara upo pale pale, lakini ukichelewa au kutofika kazini kwenye kazi yako mwenyewe ina maana tayari pato ulilotarajia kulipata limeshapungua.
Cha msingi ukiamua Kujiajiri na baadae kuajiri lazima uwe committed 100%
Ndugu zangu. Swala LA kuacha kazi linahitaji kujipanga sana, huwa siwashauri watu wakurupuke kwani yaliyonipata sipendagi na wengine yawapate
Unataka kusafiri ''huku na kule'' katika michakato ya kutengenzeza mpunga au kula bata tu? angalia baada ya bata na kumaliza savings zote, usirudi kumpigia goti tena Boss na kumwambia ''ulighafirika'' wakati unaacha kazi kwa mbwembwe. Kuacha kazi na kujiajiri haimaanishi utaacha kuhustle na kula bata full timeKwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi.
Mkuu nakuelewa vizuri. Kusafiri huku na kule bila kujali bosi atanifanya nini ni tafsiri tu ya UHURU ambao ndio ninaoutafutaUnataka kusafiri ''huku na kule'' katika michakato ya kutengenzeza mpunga au kula bata tu? angalia baada ya bata na kumaliza savings zote, usirudi kumpigia goti tena Boss na kumwambia ''ulighafirika'' wakati unaacha kazi kwa mbwembwe. Kuacha kazi na kujiajiri haimaanishi utaacha kuhustle na kula bata full time
Kwa attitude hii nakushauri mrembo usithubutu kuacha kaziMi sijui nitaacha kazi lini, kwa wiki masaa ya kufanya kazi ni masaa 8 tu!!!
Teh serious? Au wanisanifu?Kwa attitude hii nakushauri mrembo usithubutu kuacha kazi
Yaani kuacha kazi kuna nini cha kuogopeshaKwa attitude hii nakushauri mrembo usithubutu kuacha kazi