Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...

Mkuu fuata moyo wako na wala usimsikilize mtu,

Hakikisha tu unachokwenda kukifanya unakifahamu vizuri

Narudia tena fuata moyo wako

km ulifanya kazi kwa miaka 20 kwa mshahara wa laki 5 kwa mwez.... na ukashndwa kupata ivyo vitu had unastaafu....

ni uzembe pia.

Kumbuka hiyo 500000 ndo inyoendesh maisha daily
 
Kujiajiri inategemea inspiration yako, and ni vigumu kumanage business kama unafanya hivyo kwa kuiga mtu,.....
Waliofanikiwa kuacha kazi wakaingia kwny business na wakafanikiwa ni wao walikuw na mawazo hayo ya kujiajiri toka kipind wakiwa wadogo/shuleni, hawa kwao inakuwa rahisi maana anaingia kazini kwa lengo la kutafuta capital tu, mtu wa namna hii hata kwa mtaji wa mil8 tu anaweza kuwa Billionea ndan ya muda mfupi tu, hawa huwa rough sana kimwonekano hawana show off za ovyo ovyo, wanakuwa tayar kuish maisha ya kula wali maharage (buk ) wakat kaz aloacha staff tea tu buk5 , anakuwa tayar kulala chini(Hana kitanda) wakat hela ya kitanda anayo but analinda mtaji, anauwezo wa kulinda mtaji wake katika hali ngum coz anajua akiharibu itachukua muda kufika anapoenda,... kujiajiri inataka moyo but kiukwel kama una strategies unatafanikiwa, binafs niliacha chuo kabsa ili nipige biashara, mtaji unakuwa kwa kasi mpk najilaum sijui kwa nin skuishia tu f6 maana kama kiingereza kimeshakaa hesabu za hela zpo, ....ukitaka kukuza mtaji shart moja kama umeanza na mil1 ukafika mil5, usitumie faida Bali fanya hiyo mil5 yote mtaji hapo utafika mil20 then wekeza hata mil15 tena, taratibu utasogea mil50, endelea kukuza mtaji nakwambia within ten yrs mil 100 utaona pesa ya kawaida sana, kingine wakat unafanya biashara hii,unakuwa unafanya research kitu gan kingne ubaweza kufanya upanue wigo wako,..vijana wengi wanashindwa coz they know nothing about capital management in business issues, unakuta anamtaj wa mil10 AKIPATA faida yan tayar ashawaza kununua S8 edge, sijui gar, au akapange nyumba kali, ndan ya muda mfupi tu, hawajui lolote kuhusu DEAD TIME in business, hiki ni kipind ambacho hakuna faida unayoitumia zaid unakuza mtaji, haya Mambo hayahitaji shule ni natural kabsa, maana waliosomea biashara wameajiriwa kama manager, sjui account nk
Mchango wako unaelimisha na ku-inspire
 
Uzi mzuri sana huu.ninampango huu miaka mitano ijayo .kwasasa najiandaa kwa kujisomesha vikozi vya ujasiriamali mdogomdogo baada ya hapa nitafungua miradi .akili yangu inanituma nikiwa off system nitatengeneza pesa nyingi sana ambazo kwa sasa naona zinanipita kutokana na kutokuwa huru na hasa mazingira niliyopo.Mungu saidia hii ndoto itimie!
 
loading...........................................................................................................................................................................
 
Bado naona waoga wa kujiajiri ni wengi sana humu ndani..kikubwa unachotakiwa kufanya na kukikubali ni kutojali wengine watakuonaje baada ya kuacha kazi, fuata moyo na amini unachokiamini!
 
Bado naona waoga wa kujiajiri ni wengi sana humu ndani..kikubwa unachotakiwa kufanya na kukikubali ni kutojali wengine watakuonaje baada ya kuacha kazi, fuata moyo na amini unachokiamini!
Easy said than done
 
mi ni mmoja kati ya watu wenye plan ya kujilipua....

nachukia saaana kumuachia MTU muda wangu mwingi ili atengeneze faida zake.


soon nitatumia muda wangu kwa faida yangu.....

but before ya yoote... hizi ndizo nguzo muhimu.

1. miliki Nyumba 4. mbili kati ya izo ziwe maeneo mazuri kibiashara.

2. miliki mashamba si chini ya heka 50. 20 kati ya izo.... ziwe na mazao endelevu. eg. korosho... minazi... miti.. kahawa n.k

3. kuwa na mifugo... kuku..ngombe... mbuzi...nguruwe...

4. tenga mtaji wa m20 tu.....
acha kazi



hauwez juta kamwe.

mkuu upo sahihi lakini kazi zetu hizi hadi umiliki nyumba nne utakuwa umestafu na nyumba bado hazijakamilika.
wafanyakazi wengi wanajenga kwa mikopo mshaara ni ngumu sana kujenga
 
Ulifanya nini baada ya kuacha
Nilichekwa sana na kudhihakiwa hasa rafiki zangu wa karibu na ndugu yaani mtaani nilikuwa sisemi kitu ila bahati nzuri kuna wacanada walinipandilia wakawa wananilipa mkwanja wa kutosha.

Lukwafya
 
Nilichekwa sana na kudhihakiwa hasa rafiki zangu wa karibu na ndugu yaani mtaani nilikuwa sisemi kitu ila bahati nzuri kuna wacanada walinipandilia wakawa wananilipa mkwanja wa kutosha.

Lukwafya
Mkuu fafanua vizuri
 
Kwa mfanyakazi ategemeaye mshahara tu ni ndoto kufanikisha haya; Hususani wanaoishi mjini.

Ikiwa mtumishi ategemeaye mshahara ni changamoto kujenga nyumba moja tu, je ndio atakuwa na uwezo wakujenga nyumba 4 kupitia mshahara wa mwajiri wake??

Kimsingi kupata mafanikio nje ya ajira hakutegemei haya yote bali ni akiri yako tu na jinsi unavyojishughulisha.

Sababu MAISHA YAKO YANATOKANA NA UNAVYOWAZA NDANI YAKO
Mara nyingine ndio maana ukisoma mada kama hizi unazipuuza. Sasa kweli mtu ambae ajira haimridhishi unamwambia kabla ya kuacha kazi awe na nyumba nne,mashamba,mifugo na mtaji m20! Sasa si atafia kazini akitafuta hivyo vitu?!!!

Mara nyingi huwa natamani niwaambie watu jinsi nilivyoanza na mtaji mdogo saaaana lakini acha tu.
 
Mara nyingine ndio maana ukisoma mada kama hizi unazipuuza. Sasa kweli mtu ambae ajira haimridhishi unamwambia kabla ya kuacha kazi awe na nyumba nne,mashamba,mifugo na mtaji m20! Sasa si atafia kazini akitafuta hivyo vitu?!!!

Mara nyingi huwa natamani niwaambie watu jinsi nilivyoanza na mtaji mdogo saaaana lakini acha tu.
Tuambie bana mkuu utabarikiwa...kuajiriwa mizinguo!

Share with us please!
 
Back
Top Bottom