jimmyfoxxgongo
JF-Expert Member
- Jan 23, 2013
- 5,352
- 9,329
Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...
Mkuu fuata moyo wako na wala usimsikilize mtu,
Hakikisha tu unachokwenda kukifanya unakifahamu vizuri
Narudia tena fuata moyo wako
km ulifanya kazi kwa miaka 20 kwa mshahara wa laki 5 kwa mwez.... na ukashndwa kupata ivyo vitu had unastaafu....
ni uzembe pia.
Kumbuka hiyo 500000 ndo inyoendesh maisha daily