Mkuu Wolfpack ni kweli bila risk biashara haianzi. Ndio maana watu matajiri wenye mabiashara makubwa marekani kama kina Warren Buffet hutaka kufanya ubia kupunguza risk.
Hili naona kwa Tz, wanaoliweza ni ndugu zetu wa Kilimanjaro na wakinga. Na sijui kwanini watu hawapendi kufanya hata research na kwa Tz unaweza kumuliza mtu info ya biashara akakupa bure bila gharama au kama hapa jf. Na tatizo linguine kubwa ambalo linatufanya wa TZ wengi wakafeli lakini hayo makabila 2 yanaliweza ni supervision, kiukweli 75% ya wafanyakazi na supervisors ukimuajiri anataka matatizo ayamalize kwa mkupuo kabla hata mtaji haijarudshwa hata kama mmeuchukua bank haujarudi. Mfano biashara ya Bajaj nadhani mtaji hauzidi 10M sasa driver ukimpa aiendeshe anataka yeye pesa ya kwanza kukusanya kwa siku atoe 15,000 yake, wewe mwenye biashara upate 10,000 za mwisho kama zikibaki, kama hazikubaki basi akudanganye ndio maana wachaga wakaona bora wampee akusanye mfano 15M Bajaj iwe ya driver hapo Kiswahili kinakuwa hamna na hii ni kwa biashara nyingi, tuzidi kumuomba na Mungu na kuwashukuru wanaotoa mawazo endelevu.Ila jamani walimu wetu tuwasaidie wanafunzi kusoma vitabu na wanafunzi tujifunze kujisomea vitabu, hamna njia nzuri ya kujifunza kama kusoma vitabu , nawashukuru waliotoa vitabu humu. Kwa wastani mtu ukifanya mazoezi ya kawaida unaweza kusoma karatasi za vitabu mpaka karatasi 200 kwa siku bila kuleta shida kwenye ratiba yako kila siku.