Mkuu nakushukuru sana kwa kuanzisha uzi huu maalum kwa sisi tunaotaka kuacha kazi, hasa tuliopo kwenye sekta binafsi. Huku kuna manyanyaso ya kutosha...yaani ni ubabe na utemi kwa kwenda mbele. Mtu hata ukifiwa au ukawa na kikao cha harusi au familia, hupati ruhusa ya kutoka kazini.
Hapa kazini kwangu, kuna uhakika wa nyongeza ya mshahara mnano mwezi wa 8. Nasubiri mshahara upande niende benki nichukue mkopo hata wa milioni 50 niondoke hapa UTUMWANI nikajiajiri huko uraiani. Hiki kifungo cha miaka 11 kinanitosha kabisa. Kazi gani haina weekendi wala sikukuu? Kwa ujumla naichukua sana hii kazi ya shift.
Nikishachukua mkopo wangu sitajali kama nina uzoefu wa biashara au la. Nitakachofanya nitajipa takribani muda wa wiki moja nitajifungia ndani nitafakari biashara yoyote inayoweza kuniingizia kipato cha walau Tsh 20,000 kwa siku. Hata kama ni kukaanga chipsi au mihogo nitafanya ilmradi niondoke huku utumwani mwa makaburu. Kabla ya kuanza biashara yangu hiyo nitafanya business survey, ambapo nitatembea mitaani kuangalia biashara ambazo zinalipa kwa wakati huu. Hata ikibidi kujifanya kibarua wa mtu ambaye nataka kusoma biashara yake nitafanya hivyo ilmradi nipate conclusion ya ufasaha kabla sijaingia kwenye biashara husika.
Tena utafiti ngoja niuanzie hapa kwa kuwauliza wajasiriamali wenzangu (N.B: tayari najiona kama mjasiriamali mtarajiwa). Je, ndugu zangu mlionitangulia kwenye ujasiriamali, ni biashara gani ambayo nikifanya kipindi hiki cha 'vyuma kukaza' haitaniangusha? Jamani tusiwe wachoyo wa kushirikishana taarifa kwani sisi sote adui yetu ni mmoja: UMASIKINI.
Nawasilisha